Gumzo la Wiki Podcast: Waiguru ajongea UDA, naye Raila amlaumu Ruto kuhusu BBI
Listen now
Description
Je, ni kweli kuwa BBI ilichangia kukwama kwa miradi ya maendeleo? Kuna haja ya Rais Kenyatta na Odinga kuwaomba Wakenya msamaha kwa kuhujumu maendeleo kupitia BBI jinsi anavyodai Naibu wa Rais, William Ruto? Na je, ni sawa kwa Kenyatta na Odinga kumlaumu Ruto kwa kuchangia kuanguka kwa BBI au ni visingizio tu? Aidha, siasa za eneo la Kati zinazidi kuwa ngumu, Martha Karua akiteuliwa kuwa Msemaji wa Mt. Kenya Unity Forum. Ataweza? Huko Kirinyaga, Gavana Ann Waiguru aambiwa ahamie UDA ili achaguliwe tena siku chache tu baada ya Kalonzo kumtaja kuwa mmoja wa wana'OKA. Wanahabari wetu, John Mbuthia wa Nyeri, Moses Kiraese wa Pokot Magharibi na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wanatupambia makala haya.​
More Episodes
Suala la gharama ya maisha limeendelea kumkosesha Hasla usingizi! Ameamua kutumia mbinu tatu; mbolea ya bei nafuu, serikali na sekta binafsi kuagiza tani elfu miatatu za mbolea na kuagiza mahindi ili kukabili uhaba wa chakula. Atafaulu? Aidha, kuna more goodies kwa mahasla, Rais akipata fedha...
Published 12/17/22
Published 12/17/22
Uteuzi wa makatibu umezua mjadala, wana-Azimio wakilalamika kwamba Rift Valley na Mt.Kenya zimependelewa. Unadhani suala la kimaeneo lilizingatiwa? Aidha, Baba anadai Kinoti anaandamwa na anataka majasusi wa kimataifa kualikwa kushughulikia suala la mauaji ya kiholela. Riggy G naye hataki harufu...
Published 11/05/22