GUMZO LA WIKI PODCAST: Wakenya kuhusu BBI, mikopo na utapeli wa wabunge
Listen now
Description
Mapambano ya kisheria yamedhihirika katika Mahakama ya Rufaa. Hoja kuu ikiwa mwasisi hasa wa BBI ni nani. Ni Rais Kenyatta, Raila Odinga au ni Junet Mohammed na Dennis Waweru? Aidha, ripoti ya Mhasibu Mkuu wa Serikali imeweka wazi jinsi wabunge wanavyopora pesa za umma kupitia marupurupu ya usafiri. Pia, serikali inaendeleza kopakopa na mara hii Rais amekwenda kuomba bilioni 160 nchini Ufaransa huku serikali ikikosa kutii agizo la IMF kwamba ichapishe majina ya Covid-19 billionairs. Wanahabari wetu John Mbuthia wa Nyeri, said Kiraese wa Pokot Magharibi na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wanatupambia makala haya.
More Episodes
Suala la gharama ya maisha limeendelea kumkosesha Hasla usingizi! Ameamua kutumia mbinu tatu; mbolea ya bei nafuu, serikali na sekta binafsi kuagiza tani elfu miatatu za mbolea na kuagiza mahindi ili kukabili uhaba wa chakula. Atafaulu? Aidha, kuna more goodies kwa mahasla, Rais akipata fedha...
Published 12/17/22
Published 12/17/22
Uteuzi wa makatibu umezua mjadala, wana-Azimio wakilalamika kwamba Rift Valley na Mt.Kenya zimependelewa. Unadhani suala la kimaeneo lilizingatiwa? Aidha, Baba anadai Kinoti anaandamwa na anataka majasusi wa kimataifa kualikwa kushughulikia suala la mauaji ya kiholela. Riggy G naye hataki harufu...
Published 11/05/22