Gumzo la Wiki Podcast: Usalama Laikipia; siasa za 2022-Wakenya wazungumza
Listen now
Description
Suala la usalama huko Laikipia linazidi kuwa kero huku wanasiasa wakilaumiwa kuchochea hali hiyo. Je, nani wa kulaumiwa kufuatia kudorora kwa usalama? Ruto naye amemjibu Matiang'i kuwa iwapo anadhani ana ardhi Laikipia, basi awagawie wakazi. Katika ulingo wa siasa, Mlima Kenya imekuwa kama msichana mrembo anayemezewa mate huku kila anayetaka kuwania urais akitafuta mgombea mwenza huko. Nani awe mgombea mwenza wa nani? Aidha, viongozi wameanza ujanja wa kuwa karibu na Mkenya huku Raila akitumia usafiri wa umma. Kadhalika, CBC imewafikia kooni wazazi kutokana na mazoezi ya ajabu wanayowasaidia wanao kufanya. Wanahabari wetu, Moses Kiraese wa Pokot Magharibi na John Mbuthia wa Nyeri wanatupambia makala haya.
More Episodes
Suala la gharama ya maisha limeendelea kumkosesha Hasla usingizi! Ameamua kutumia mbinu tatu; mbolea ya bei nafuu, serikali na sekta binafsi kuagiza tani elfu miatatu za mbolea na kuagiza mahindi ili kukabili uhaba wa chakula. Atafaulu? Aidha, kuna more goodies kwa mahasla, Rais akipata fedha...
Published 12/17/22
Published 12/17/22
Uteuzi wa makatibu umezua mjadala, wana-Azimio wakilalamika kwamba Rift Valley na Mt.Kenya zimependelewa. Unadhani suala la kimaeneo lilizingatiwa? Aidha, Baba anadai Kinoti anaandamwa na anataka majasusi wa kimataifa kualikwa kushughulikia suala la mauaji ya kiholela. Riggy G naye hataki harufu...
Published 11/05/22