Gumzo la Wiki Podcast; OKA yafufuka, Jubilee ikiwaka moto
Listen now
Description
Imekuwa wiki yenye matukio kadhaa ya kisiasa huku muungano wa OKA ulioonekana kufifia ukifufuka kwa mikutano ya kuwatia wasiwasi wapinzani japo swali ni lile lile la ni nani atakayepata tikiti? Kule Jubilee, mikakati ya kumtema Ruto rasmi inaendelea huku naye akiendeleza cheche kali, wakati huu akikosoa mikopo waliyoichukua kwa pamoja na Rais Kenyatta. Wanafunzi nao wamefanikiwa kuishinikiza serikali kuwapa likizo. Ndiyo suluhu ya mioto shuleni? Moses Kiraese wa Pokot Magharibi, William Omasire wa Nyamira na Martin Ndiema wa Trans Nzoia wanatupambia sehemu hii.
More Episodes
Suala la gharama ya maisha limeendelea kumkosesha Hasla usingizi! Ameamua kutumia mbinu tatu; mbolea ya bei nafuu, serikali na sekta binafsi kuagiza tani elfu miatatu za mbolea na kuagiza mahindi ili kukabili uhaba wa chakula. Atafaulu? Aidha, kuna more goodies kwa mahasla, Rais akipata fedha...
Published 12/17/22
Published 12/17/22
Uteuzi wa makatibu umezua mjadala, wana-Azimio wakilalamika kwamba Rift Valley na Mt.Kenya zimependelewa. Unadhani suala la kimaeneo lilizingatiwa? Aidha, Baba anadai Kinoti anaandamwa na anataka majasusi wa kimataifa kualikwa kushughulikia suala la mauaji ya kiholela. Riggy G naye hataki harufu...
Published 11/05/22