Description
Mswada wa Marekebisho ya Sheria za Vyama vya Kisiasa umekuwa kichocheo cha mjadala wiki hii, ambapo wengi wanajiuliza iwapo kufaulu kwake kutakuwa mwanzo wa wanasiasa kuaminiana.
Je, iwapo mswada huo utafanywa sheria, tutarajie miungano gani, hasa kati ya nani na nani?
Na je, mswada huu umeashiria upande gani kuwa na ubabe bungeni?
Aidha, tunaangazia mwaliko wa Ruto kwa kina Mudavadi na Wetangula licha ya kusema hawajaalikwa wala kukutana na yeyote kujadili miungano.
Je, kuna karata gani ambayo inachezwa na wanasiasa hawa kuelekea uchaguzi mkuu wa Agosti 9 mwaka huu.
Vilevile mjadala kuhusu haja ya wanafunzi kufanyiwa vipimo vya kubaini iwapo wanatumia dawa za kulevya au la kabla ya kurejea shuleni. Je, unafikiri hatua hii itasaidia kudumisha nidhamu shuleni?
Wanahabari wetu Faith Kutere wa Eldoret, Bernard Lusigi wa Kakamega na Moses Kiraese wa Pokot Magharibi wameshiriki gumzo na wananchi kuhusu masuala haya.