Machungu yakumbayo wahamiaji na wakimbizi njia za ardhini ni makubwa kuliko baharini Mediteranea
Listen now
Description
Ripoti mpya ya mashirika ya Umoja wa Mataifa yabaini kuwa wahamiaji na wakimbizi wanaotaka kuelekea Ulaya kusaka maisha bora kupitia njia za ardhini Afrika, wanakumbwa na ukatili sio tu wanapokuwa baharini, bali pia ardhini wanapokatiza nchi zingine kuelekea fukwe za bahari ya Mediteranea. Bosco Cosmas na maelezo zaidi. Ikipatiwa jina Katika safari hii hakuna anayejali unaishi au unakufa, ripoti imeandaliwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na la wahamiaji, IOM kwa ushirikiano na lile la Kimataifa la Wahamiaji Mseto (MMC). Ripoti inasema wakimbizi na wahamiaji wanazidi kupita maeneo ya ardhini ambako makundi ya waasi, wanamgambo na wahalifu wengine wanafanya kazi, na ambapo biashara haramu ya binadamu, utekaji nyara kwa ajili ya kikombozi, utumikishwaji kwenye kazi na ukatili wa kingono umeenea. Hayo yanatokea wakati inakadiriwa kuwa watu wengi huvuka zaidi kulekea Ulaya kupitia jangwa la Sahara kuliko bahari ya Mediterania huku vifo vya wakimbizi na wahamiaji jangwani vikidhaniwa kuwa ni maradufu zaidi ya vile vinavyotokea kwa wanaovuka kupitia bahari ya Mediterania huku ikionya juu ya ongezeko kubwa la watu wanaojaribu kuvuka eneo hilo hatari. Licha ya ahadi zinazofanywa na Jumuiya ya Kimataifa kuokoa maisha na kushughulikia udhaifu unaondelea, kwa mujibu wa sheria za kimataifa, mashirika hayo matatu yanaonya kwamba hatua za sasa za Kimataifa hazitoshi kutokana na mapungufu makubwa kwenye ulinzi katika njia ya kati ya Mediterania. Yanachotaka sasa mashirika hayo ni ulinzi mahsusi kulingana na njia wanazotumia wakimbizi na wahamiaji ili kuokoa maisha, kupunguza machungu na kung’oa mzizi wa kile kinachosababisha watu kukimbia nchi zao kwa kusaka mbinu bora za ujenzi wa amani.  
More Episodes
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, hususan jimboni Kivu Kaskazini kwenye mji mkuu, Goma, Alhamisi ya Oktoba 3 iligubikwa na kiza nyakati za asubuhi baada ya boti kuzama kwenye Ziwa Kivu. Ilikuwa inasafiri kutoka Minova, jimboni Kivu Kusini. Zahma hii imesababisha vifo kwa mujibu wa...
Published 10/04/24
Washiriki wa hafla ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Walimu ililofanyika leo Oktoba 4 katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) jijini Paris, Ufaransa  wamesisitiza wito wa kuthamini mawazo ya walimu katika kuboresha elimu ya ulimwengu.  Kama...
Published 10/04/24