DRC ni zaidi ya muziki, tutatumia Kiswahili kueneza utamaduni wetu - Balozi Ngay
Listen now
Description
Kufuatia lugha ya Kiswahili kutambuliwa na Umoja wa Mataifa na kutengenewa siku maalum, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC sasa imesema itajengea uwezo wasanii wake wanaoimba kwa lugha ya Kiswahili kama njia mojawapo ya kusambaza utamaduni wa taifa hilo. Mwakilishi wa Kudumu wa DRC kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Zénon Mukongo Ngay amesema hayo katika ujumbe wake kupitia Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa. Ikumbukwe kuwa tarehe 1 Julai mwaka huu Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio la kutangaza tarehe 7 Julai kuanzia mwaka huu kuwa siku ya Kiswahili dunia na kutaka nchi wanachama na wadau pamoja na mashirika kuchukua hatua kusongesha lugha hiyo ya 10 kwa kuwa na wazungumzaji wengi zaidi duniani, kwa mujibu wa UNESCO. Balozi Ngay kwenye ujumbe wake amesema DRC imefurahishwa na kitendo cha Kiswahili kutambulika katika kiwango cha kimataifa. DRC ni zaidi ya muziki, tutatumia kiswahili kueneza utamaduni wetu “Siku ya Julai 7 itabakia katika kumbukumbu. Kiswahili ni lugha itakayokuwa chombo cha biashara duniani kote, ni jambo la kujivunia,” amesema Balozi Ngay. Ametanabaisha kuwa DRC ni mashuhuri si katika muziki peke yake, akisema utamaduni wa DRC ni mkubwa, muziki ni kipengele kimoja tu cha utamaduni wetu. Amesema idadi kubwa ya wakongomani wanaoimba kwa lugha ya kiswahili wameingia kwenye injili na nyimbo zao nyingi zinatambulika kwenye sehemu ya eneo la Mashariki mwa Afrika. Tutahimiza matumizi ya Kiswahili kweney muziki wa kijamii Kwa kuzingatia uzito wa sasa wa Kiswahili, DRC pia itahimiza matumizi ya lugha hiyo katika kile kinachoitwa muziki wa kijamii. Balozi Ngay amesema watakachofanya wao sasa ni kukuza wasanii wanaoweza kuimba kwa lugha ya Kiswahili. Tarehe 1 Julai mwaka huu wa 2024 Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha Azimio (A/78/L.83) la kutambua Julai 7 kuwa Siku ya Kimataifa ya Kiswahili. Awali siku hii ilikuwa inatambuliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO kupitia azimio lililopitishwa mwezi Novemba mwaka 2021.
More Episodes
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, hususan jimboni Kivu Kaskazini kwenye mji mkuu, Goma, Alhamisi ya Oktoba 3 iligubikwa na kiza nyakati za asubuhi baada ya boti kuzama kwenye Ziwa Kivu. Ilikuwa inasafiri kutoka Minova, jimboni Kivu Kusini. Zahma hii imesababisha vifo kwa mujibu wa...
Published 10/04/24
Washiriki wa hafla ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Walimu ililofanyika leo Oktoba 4 katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) jijini Paris, Ufaransa  wamesisitiza wito wa kuthamini mawazo ya walimu katika kuboresha elimu ya ulimwengu.  Kama...
Published 10/04/24