04 OKTOBA 2024
Listen now
Description
Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini Lebanon, na kesho ikiwa ni Siku ya walimu Dunia tunakupeleka Paris, Ufaranza kutsikia toka UNESCO. Makala tunafuatili ajali ya boti iliyozama katika ziwa Kivu nchini DRC na mashinani tunakupeleka Burundi, kulikoni?  Mashirikika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo yameonya kwamba hali ya kibinadamu inazidi kuwa mbaya nchini Lebanon wakati mashambulizi ya anga ya Israel yakiendelea kushika kasi na kuwafungisha virago maelfu ya watu, wengi wakikimbia nchi jirani ya Syria ambako nako si shwari.Washiriki wa hafla ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Walimu ililofanyika leo Oktoba 4 katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) jijini Paris, Ufaransa  wamesisitiza wito wa kuthamini mawazo ya walimu katika kuboresha elimu ya ulimwengu.Makala inakupeleka huko Goma, jimboni Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako janga la kuzama kwa boti ya abiria na mizigo liligubika eneo hilo Alhamisi asubuhi za huko.Na mashinani kupitia video ya WHO Afrika, tunamsikia Dkt. Dieudonné Niyongere akizungumza kuhusu msaada muhimu wa washirika katika kuimarisha juhudi za kukabiliana na mlipuko wa Mpox nchini Burundi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu! 
More Episodes
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, hususan jimboni Kivu Kaskazini kwenye mji mkuu, Goma, Alhamisi ya Oktoba 3 iligubikwa na kiza nyakati za asubuhi baada ya boti kuzama kwenye Ziwa Kivu. Ilikuwa inasafiri kutoka Minova, jimboni Kivu Kusini. Zahma hii imesababisha vifo kwa mujibu wa...
Published 10/04/24
Washiriki wa hafla ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Walimu ililofanyika leo Oktoba 4 katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) jijini Paris, Ufaransa  wamesisitiza wito wa kuthamini mawazo ya walimu katika kuboresha elimu ya ulimwengu.  Kama...
Published 10/04/24