22 OKTOBA 2024
Listen now
Description
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini DRC kufuatilia kazi za kituo cha Taifa cha Redio na Televisheni, RTNC huko Beni jimboni Kivu Kaskazini za kakabiliana na habari potofu. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani. Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo mjini Cairo, Misri, imebainisha kwamba athari za vita zimerudisha nyuma maendeleo huko Gaza kwa takriban miaka 69. Ripoti hiyo iliyoratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP na  Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Kiuchumi na Kijamii kwa Asia Magharibi imeonya kwamba bila kuondoa vikwazo vya kiuchumi na kuwekeza katika maendeleo, uchumi wa Palestina unaweza kushindwa kurejesha viwango vya kabla ya vita na kusonga mbele kwa kutegemea misaada ya kibinadamu pekee.Kiongozi wa timu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) ya kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa Marburg Dkt. Janet Diaz ameeleza kwamba uongozi thabiti wa serikali ya Rwanda umewezesha kufanya uamuzi wa haraka na kuchukua hatua kuanzisha mwitikio wa sekta mbalimbali dhidi ya mlipuko wa sasa wa ugonjwa huo wa Marburg nchini humo.Na uongozi wa Kikosi cha Muda cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon (UNIFIL) umeendelea kusisitiza kwamba pamoja na changamoto zilizopo, walinda amani wa UNIFIL wanaendelea kufanya kazi kwa karibu na jamii za kusini mwa Lebanon ili kuwezesha utoaji wa misaada ya kibinadamu kwa wenye uhitaji. Hivi karibuni kumekuwa na mashambulizi dhidi ya walinda amani hao wa Umoja wa Mataifa yanayotekelezwa na majeshi ya Israeli.Mashinani kupitia video ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya Kibinadamu na misaada ya dharura OCHA tunamuangazia mmoja wa watu waliokimbia makazi yao akiwa katika shule ya Al Rimal, akielezea changamoto wanazokutana nazo katika kukabiliana na hali ngumu inayowakabili raia wa Gaza.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 
More Episodes
Umoja wa Mataifa unaendelea kuunga mkono serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC katika kukabili habari potofu na za uongo hususan huko mashariki mwa nchi ambako vikundi vilivyojihami vinaendelea kushambulia raia na kupambana na jeshi la serikali. Hivi karibuni Umoja wa Mataifa kupitia...
Published 10/22/24
Kaunti ya Turkana Kaskazini mwa Kenya moja ya maeneo kame mradi wa ufugaji nyuki wa WFP umekuwa mkombozi kwa wakulima walioathirika na mabadiliko ya tabianchi. Katika kaunti hii vumbi linalotimuka katika eneo tambarare lisilo na miti linakufanya kujiuliza je Nini kizuri kinaweza kufanyika hapa...
Published 10/21/24