Description
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, (WFP) leo kwa mara nyingine tena limetahadharisha kwamba bila msaada wa kibinadamu nchini Sudan, mamia ya maelfu wanaweza kufa kwa njaa.
Vita vya kikatili nchini Sudan vimesababisha janga kubwa zaidi la njaa duniani, imeandika WFP katika ukurasa wake wa X leo Oktoba 28 na kufafanua zaidi kwamba mtu mmoja kati ya watu wawili nchini humo anatatizika kupata mlo kila siku.
WFP inaeleza kuwa njaa imethibitishwa Kaskazini mwa Darfur na mahitaji ya kibinadamu ni makubwa sana.
Kabla ya taarifa hii ya leo ya WFP, jana kupitia pia ukurasa wa mtandao wa X, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Cindy McCain ambaye hivi karibuni alikuwa Sudan mojawapo ya maeneo yenye njaa zaidi duniani, ambapo watu milioni 25 wanakabiliwa na njaa kali ameandika kwamba WFP iko Sudan inatoa msaada wa kuokoa maisha lakini wanahitaji kwa haraka mambo matatu ambayo ni kuwafikia watu ili kuwasaidia, misaada kuweza kupita katika kila kivuko na usaidizi zaidi wa kimataifa kwa Wasudani walio katika mazingira hatarishi.
Kwa miaka mingi, Sudan imekuwa ikisumbuka na migogoro. Mgogoro wa hivi karibuni zaidi, ulioanza Aprili mwaka jana 2023, umezua janga baya zaidi duniani la watu kuhama makwao na janga kubwa zaidi la njaa duniani linalosambaa Sudan, Sudan Kusini na Chad.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Geneva Uswisi kuwasikia vijna kutoka Kenya ambao wanashiriki kongamano la vijana, wakieleza kuhusu mkataba wa zama zijazo na mchango wao katika kuutekeleza mashinani mwao. Pia tunakuletea muhtasari wa habar iza Sudan, Kura ya Knesset kuhusu...
Published 10/29/24
Kampuni ya Craftskills Wind Energy International Limited wamiliki wa mradi wa nishati ya umeme itokanayo na upepo ya Kipeto Energy iliyoko Kaunti ya Kajiado nchini Kenya wamejitwalia tuzo ya “Mtu Bora wa Mwaka wa Umoja wa Mataifa. 2024”
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo anasema ushindi huo ni...
Published 10/28/24