29 OKTOBA 2024
Listen now
Description
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Geneva Uswisi kuwasikia vijna kutoka Kenya ambao wanashiriki kongamano la vijana, wakieleza kuhusu mkataba wa zama zijazo na mchango wao katika kuutekeleza mashinani mwao. Pia tunakuletea muhtasari wa habar iza Sudan, Kura ya Knesset kuhusu UNRWA, na Siku ya kimataifa ya huduma, na mashinani. Baada ya Bunge la Israel hapo jana Oktoba 28 kupiga kura ya kuizuia Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) kufanya shughuli zake katika maeneo yote yaliyoko chini ya Israel, viongozi wa Umoja wa Mataifa kuanzia Katibu Mkuu Antonio Guterres wameendelea kupaza sauti kwamba kuizuia UNRWA ni ukiukwaji wa sheria za kimataifa na italeta zahma kwa maisha ya watu katika eneo hilo la Mashariki ya Kati. Katibu Mkuu Guterres amesema analileta suala hili kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, na atahakikisha Baraza hilo muda wote linakuwa na taarifa kwa kadri hali inavyoendelea.Ujumbe Huru wa Kimataifa wa Umoja wa Mataifa  wa kutafuta ukweli nchini Sudan umesema katika ripoti yake mpya ya kina leo kwamba Vikosi vya wanamgambo wa RSF, ambavyo vimekuwa vikipigana na Jeshi la Sudan (SAF) katika mzozo unaoendelea nchini humo, vinahusika na kufanya ukatili wa kingono kwa kiasi kikubwa katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wao, ikiwa ni pamoja na ubakaji wa makundi na kuwateka nyara na kuwaweka kizuizini waathiriwa katika hali ambayo ni sawa na utumwa wa ngono.Na leo ikiwa ni Siku ya Kimataifa ya Usaidizi na Matunzo, makadirio mapya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi (ILO), yaliyotolewa leo yanaonesha takribani wanawake milioni 708 duniani kote wako nje ya nguvu kazi zenye ujira kwa sababu ya majukumu ya kutoa usaidizi au matunzo bila malipo. Utafiti huo umefanywa katika nchi 125.Mashinani leo tutakwenda katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Al Matar huko Kassala, Sudan, kusikiliza ujumbe kutoka kwa Ted Chaiban, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, aliyefanya ziara kambini humo.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 
More Episodes
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, (WFP) leo kwa mara nyingine tena limetahadharisha kwamba bila msaada wa kibinadamu nchini Sudan, mamia ya maelfu wanaweza kufa kwa njaa.  Vita vya kikatili nchini Sudan vimesababisha janga kubwa zaidi la njaa duniani, imeandika WFP katika...
Published 10/28/24
Kampuni ya Craftskills Wind Energy International Limited wamiliki wa mradi wa nishati ya umeme itokanayo na upepo ya Kipeto Energy iliyoko Kaunti ya Kajiado nchini Kenya wamejitwalia tuzo ya “Mtu Bora wa Mwaka wa Umoja wa Mataifa. 2024” Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo anasema ushindi huo ni...
Published 10/28/24