Episodes
Katika makala haya tunajadili haki za mtoto kupata elimu nchini DRC, hapa mkuu wa chuo cha walumu cha ISP, Butua Balingane anafafanua vizingiti vya mtoto kupata elumu nchini DRC.
Published 11/12/24
Published 11/12/24
Nchini DRC, kumeripotiwa upungufu wa watoto wa kike katika kupata elimu, hili likidaiwa kuchangiwa na tamaduni zilizopitwa na wakati.
Published 11/05/24
Nchini Kenya, idara ya polisi imekiri kwamba wanawake 97 wameuawa kwa kipindi cha miezi 3, baadhi miili yao ikipatikana imenyofolewa.
Published 11/05/24
Nchini Kenya, visa vya raia kutekwa na kisha baadaye kuachiliwa au kupatikana wameuawa vinazidi kuongezeka, visa kadhaa vikiendelea kugonga vichwa vya habari.
Published 10/25/24
Katika muendelezo wa makala kuhusu siku ya mtoto wa kike duniani,  tunaangazia vyanzo vya visa vya unyanyasaji wa watoto wa kike na hatua zilizopigwa na mashirika mbalimbali katika kuifanya sauti ya mtoto wa kike kusikika.
Published 10/24/24
Siku ya Mtoto wa Kike Duniani, inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 11 Oktoba, ni fursa ya kuangazia changamoto zinazokabili watoto wa kike duniani na kukuza usawa wa kijinsia.
Published 10/18/24
Chakula ni muhimu kwa maisha, kuishi, heshima, ustawi, na maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa  watu binafsi, jamii, na mataifa. Sheria za kimataifa zinatambua haki ya kila mtu kupata chakula cha kutosha na haki ya kuwa huru kutokana na njaa. Haki hii ni ya msingi kwa utekelezaji wa haki zote za binadamu.
Published 10/16/24
Katika makala haya tunaangazia ripoti ya umoja wa mataifa kusema kwamba zaidi ya wanawake wafungwa ya 260 walibakwa katika jela ya Makala nchini DRC, mapema mwezi huu wakati wa jaribio la wafungwa kutoroka jela.
Published 09/19/24
Nchini Kenya zaidi serikali inaendesha uchunguzi wa chembechembe za DNA, za wanafunzi 21 wa shule ya msingi ya Endatasha baada yao kuteketea kiasi ya kutotambulika, kabla ya miili yao kutolewa kwa familia.
Published 09/16/24
Katika makala haya tunajikiti kuangazia uketetetaji ambapo wasichana  wamekuwa ukiendelea kukeketewa nchini Kenya licha ya serikali kanzisha kampeni ya kuhamasisha umma kuhusu athari zinazotokana na ukeketaji huo.
Published 08/27/24
Jamii zinazoishi mikapani nchini Kenya kwa muda zimekuwa  zikikosa huduma muhimu ya kupata vitambulisho kutoka na sababu ambazo wenyewe wanasema serikali inawabagua.
Published 08/24/24
Katika makala haya saba yetu inalenga taifa la Tanzania eneo la Ngorongoro ambapo serikali imekuwa ikiwahamisha wenyeji eneo hilo, ili kuihifadhi eneo hilo  kutokana na historia yake.
Published 08/06/24
Katika makala haya tunajadili haki za kina dada pamoja na kina dada wanaojiuza.
Published 08/03/24
Juma hili tunaangazia haki za wanahabari kupeperusha habari zao bila kuingiliwa na vyombo vya usalama katika mataifa yao.
Published 07/27/24
Katika makala haya tunaangazia dhuluma zinazodaiwa kutekelezwa na wanajeshi wa Uingereza ambao wana kambi ya mazoezi nchini Kenya leo la Nanyuki.
Published 07/16/24
Visa vya dhuluma dhidi ya wanawake vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara katika jamii mbalimbali barani Afrika na hata duniani,jambo ambalo limechangia sheria nyingi kuanzishwa kulinda wanawake,lakini hata hivyo dhuluma hizo zimeanza kuwakumba wanaume wengi kwa kunyanyaswa na kupingwa na wake wao.
Published 07/10/24
Taifa la Sudan Kusini linashuhudia wimbi kubwa la wakimbizi wanaoendelea  kukimbia vitra nchini Sudan, licha taifa hilo kuendelea kushuhudia changamoto nyingi tu ikiwemo ukosefu wa amani katika baadhi ya majimbo yake.
Published 07/06/24
Nchini Kenya vijana  wamekuwa wakiandamana kulalamikia kile wataja mpango wa serikali kuongeza kodi kwa kutumia mswada wa fedha wa mwaka 2024.
Published 06/25/24
Idadi ya watu waliopewa adabu ya kifo iliongezeka zaidi mwaka 2023, mataifa ya mashariki ya kati na nchini Somalia abadu hiyo ikiripotiwa kuwa ya juu zaidi.
Published 06/18/24
Katika makala  haya ni awamu ya pili tunaendelea na mazungumzo yetu na bwana meshaka Sisende raia wa Kenya anayeishi na ulemavu wa ngozi.
Published 06/17/24
Kila mwaka Juni 14 dunia huadimisha siku ya watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi sherehe zilizoanza kuadimisha tangu mwaka 2014, ili kuhamasisha jamii kwamba watau wanaoishi na ulemavu wa ngozi wao ni watu wa kawaida katika jamii.
Published 06/12/24
Makala haya yanaangazia tendekazi wa tume za kutetea haki za biandamu za serikali zetu za Africa mashariki. Hii ni baada ya lalama kutoka kwa kiongozi wa upinznai nchini Uganda, Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine kwamba tume ya haki nchini Uganda imekuwa ikiegemea upande wa serikali katika kutekeleza majukumu yake.
Published 05/31/24
Katika makala haya tunaangazia haki za kina dada ambao hawajafanikiwa kupata watoto katika jamii zetu za kiafrica.  Barani Afrika wanawake ambao hawana uwezo kupata watoto au  wale  huchukuwa muda mrefu kupata watoto , hupitia changamoto si haba ,na kukosa haki,kama vile kutotambuliwa na jamii,uridhi wa Mali na hata wengine kufukuzwa kwenye ndoa,hali hiyo ikichochewa na tamaduni ambazo zimekita mizizi.
Published 05/21/24
Nchini DRC ; familia ya jamii ya  mbilikimo , ukipenda wambute kama wanavyo  wanavyofahamika nchini DRC, wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukiukaji wa haki za binadamu.
Published 05/18/24