Ufahamu zaidi Mradi wa Kuendeleza Utalii Kusini mwa Tanzania - REGROW
Listen now
Description
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii inatekeleza mradi wa kukuza utalii kusini mwa Tanzania (REGROW). Mradi wa REGROW ni mkopo kutoka Benki ya Dunia na lengo kuu la mradi huu ni kuboresha maeneo yenye vivutio vya utalii katika ukanda wa kusini mwa Tanzania. Hii ni pamoja na kuboresha usimamizi wa maliasili na kuimarisha fursa za kiuchumi kwa wananchi wanaozunguka hifadhi ili kuongeza mchango wa sekta ya utalii katika maendeleo ya kiuchumi nchini . Serikali inadhamiria mradi huu uwe wa mfano katika kuleta maendeleo kwa kufungua fursa za kiuchumi kwa jamii na taifa kwa ujumla.