MJASIRIAMALI LAZIMA AELEWE MAMBO HAYA
Listen now
Description
.Habari rafiki mpendwa, natumaini unaendelea vizuri na mapambano ya maisha.Nikutie tu moyo endelea na harakati hizo naamini ipo siku utayaona matunda ya unachokifanya.Kama kawaida leo nakuletea makala nyingine hii ni juu ya sifa za mjasiriamali. Kuna watu wengi sana wanajiita wajasiriamali lakini kiuhalisia si wajasiriamali.Hii imenifanya nifikirie juu ya hili. Zifuatazo ni sifa za mjasiriamali na kama huna sifa kati ya hizi basi hujawa mjasiriamali wa ukweli bali utakuwa unabip tu. sifa zenyewe ni kama zifuatazo, 1. AWE NA MALENGO Hii ni sifa kubwa ambayo mjasiriamali anatakiwa kuwa nayo, kwanza lazima uwe na malengo uliyojiwekea kwamba unataka kufikia wapi katika biashara yako.kama ni kuwa na pesa nyingi sema unataka kiasi gani kabla ya mwaka kuisha.kwa mfano; nataka kabla ya mwaka 2016 kuisha niwe nimetengeneza Milioni 20.Hii itakufanya ufanye kazi kwa bidii ili ufikie malengo hayo. 2. AWE NI MTU ASIYE KATA TAMAA. Mjasiriamali yoyote duniani ni mtu ambaye si rahisi sana kukata tamaa katika kazi zake, watu wengi sana wamekuwa na malengo makubwa lakini wanashindwa kuyafikia kwasababu wanakata tamaa mapema sana,hii huwafanya warudi nyuma.Mfano mtu aliyeajiriwa anakuwa na malengo ya kujiajiri, anaanzisha biashara asipopata faida kama alivyotarajia hukata tamaa na kutamani tena kuajiriwa na hatimaye kutafuta ajira tena.Nikutie moyo tu hakuna kitu kinachokuja kwa urahisi kama unavyofikiria,kaza buti songa mbele changamoto ni chachu ya mafanikio. 3. AWE NI MTU WA KUJIAMINI. Siku zote anayejiamini ndio hupata mafanikio kwa urahisi, watu wengi wamekuwa wakishindwa katika biashara zao kwa kushindwa kujiamini.Kumbuka hiyo ni biashara yako acha kuangalia watu wanasema nini wewe endelea tu na harakati zako ipo siku hao wanaokubeza watakusifia kwa unachokifanya. 4. KUJALI MUDA WAKO. Muda ni kitu kidogo sana lakini muhimu kuliko kitu chochote, mbaya zaidi dakika moja au hata sekunde moja kupita hatokutana nayo tena katika mzunguko wa maisha yako yote.Kwahiyo kama umekuwa na malengo ya kufanya kitu fulani basi fanya haraka iwezekanavyo, ukizidi kuchelewa unaendelea kuweka matatizo na vikwazo katika kazi yako au hata biashara yako kuna msemo unasema"muda ni mali" au "time is money". Misemo hii imefananisha muda ni pesa, kwasababu pesa ni kitu muhimu lakini utapata pesa kwa kutumia muda vizuri.Acha kuahirisha mambo mara kwa mara fanya maamuzi sasa, kesho kamwe haitafika. 5. AWE NA KAULI NZURI, TABASAMU NA NADHIFU. Hii ni nguzo muhimu sana kwa mjasiriamali, unapokuwa na kauli nzuri na mwenye tabasamu na nadhifu, unapokuwa unatoa huduma utawavutia wateja wengi zaidi na kama utakuwa na kauli mbaya na mchafu wateja watakimbia na mwisho wa siku unaanza kufikiria umelogwa kumbe wewe ndiye mchawi namba moja wa biashara yako. Zingatia hilo na utaona utakavyopata wateja kuliko kawaida.
More Episodes
Mziki mzuri na maelezo ya wasani mbalimbali yana patikana hapahapa jamsingi subscribe ili uwe wa kwanza kupata vibes connection
Published 11/16/20
Published 11/16/20
"COUNTRY BOY" AZUNGUMZIA UMUHIMU WA MSANII KUWA TRENDING YOUTUBE NA VIEWS WENGI KWENYE MUZIKI WAKE.
Published 11/10/20