Episodes
Mziki mzuri na maelezo ya wasani mbalimbali yana patikana hapahapa jamsingi subscribe ili uwe wa kwanza kupata vibes connection
Published 11/16/20
Published 11/16/20
"COUNTRY BOY" AZUNGUMZIA UMUHIMU WA MSANII KUWA TRENDING YOUTUBE NA VIEWS WENGI KWENYE MUZIKI WAKE.
Published 11/10/20
Karibu kwa mara nyingine tena kusikiliza show yako matata una weza ku subscribe ili kuwa wakwanza kupata burudani .
Published 11/02/20
Karibu sana endelea kupata burudani ya connection vibes ya Msasaonline. Ukibonyeza www.msasaonline.co utafurahia show
Published 10/24/20
Connection vibes ni bonge la kipindi ambacho ni collection ya story zote za burudani ambacho hupatikana www.msasaonline.com
Published 10/18/20
wwwmsasaonline.co
Published 10/12/20
KARIBU KWA MARA NYINGINE TENA KWENYE MWENDELEZO WA EPISODE ZA CONNECTION VIBES KIUNDANI ZAIDI BONYEZA www.msasaonline.co ili uweze kuala unapatamwendelezo subscribe
Published 10/03/20
KARIBU SANA UBURUDIKE NA CONNECTION VIBES YA MSASAONLINE KWA TAARIFA NA BURUDANI TEMBELEA  WWW.MSASAONLINE.CO
Published 09/26/20
KARIBU UBURUDIKE NA CONNECTION VIBES
Published 09/19/20
Haijalishi uko wapi, unaishi wapi, wewe ni nani na unafanya nini. Ila ukweli ni kuwa kila mmoja wetu ana masaa 24 kwa siku. Na katika masaa hayo hayo tunatumia kwa kupumzika na kufanya mambo mbalimbali katika maisha. Moja kati ya maswali mwanadamu amekua akijiuliza mara kwa mara, ni kutaka kufahamu dhumuni la maisha yake hapa duniani. Tumekua tukijiuliza mimi ni nani? kwanini nipo hapa duniani?.Na katika kutafakari huko ndipo wengi wetu tunafikiria kuhusu kazi au wito wetu. Kwani kuna...
Published 08/31/20
Neno mafanikio kila mtu huwa ana maana yake kwa wakati wake na kwa eneo lake katika maisha. Nikiwa na maana kuwa kila mtu ana tafsiri yake kuhusu mafanikio kutokana na muda na wakati alionao na anaoendelea kuishi hapa duniani. Mfano : kuna mafanikio ya kiafya, kiuchumi, kiuchumi, kimahusiano. Sasa katika makala yetu leo hii tutazungumzia zaidi juu ya Mafanikio ya kiuchumi na kifedha. Hizi ni Siri muhimu ambazo ni nguzo kuu za kukusaidia kufikia Mada makubwa kiuchumi na kifedha. 1. IMANI...
Published 08/31/20
Nidhamu ni utii, kusikia, na kusikiliza. Nidhamu ni kufuata sheria, kanuni na taratibu kutoka kwa wanaokuongoza. Nidhamu ni kuwa mahala sahihi, wakati sahihi na kufanya jambo lililokuhitaji kuwa mahala pale kwa wakati ule. Nidhamu sio shikamoo, nidhamu sio upole na nidhamu sio Mavazi yenye staha pekee. Nidhamu ni zaidi ya mwonekano nadhifu na mavazi adili. Nidhamu ni mwenendo chanya, tabia nzuri, fikra chanya na kauli jengefu. Taaluma ni maarifa, ujuzi na mjongeo fulani wa fikra unaokuwa...
Published 08/31/20
Kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps amesema kiungo wa kati wa klabu ya Manchester United, Paul Pogba amepatikana na maambukizi ya Virusi vya Corona. Kutokana na taarifa hiyo Pogba mwenye umri wa miaka 27 atalazimika kujitenga na wachezaji wenzake ambao wapo kwenye maandalizi ya michuano ya ligi ya Taifa la Ufaransa. Kwahiyo mfaransa huyo atakosa mechi ya kitaifa ya Ufaransa itakayochezwa siku ya Jumamosi tarehe 5 Septemba, 2020 na siku 3 baadae atakosa kwenye mechi dhidi ya...
Published 08/28/20
MAMLAKA ya Mwasiliano Tanzania (TCRA) imeagiza Clouds TV na Redio kusitisha matangazo yao kwa muda wa siku saba kuanzia kesho Ijumaa 28 Agosti hadi 3 Septemba 2020 kwa kosa la kukiuka kanuni za utangazaji na kanuni ndogo za utangazaji za uchaguzi. Pia, mamlaka hiyo imevitaka Clouds TV na Redio kuomba radhi siku nzima ya leo Alhamisi tarehe 27 Agosti 2020 kwa kosa hilo. Akizungumza na waandishi wa habari makamo makuu ya mamlaka hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba amesema, adhabu...
Published 08/28/20
Katika jitihada za kudhibiti maambukizi ya Covid-19, Rais Uhuru Kenyatta ameongeza muda wa wananchi kutotoka ndani kuanzia saa 3 usiku hadi saa 10 alfajiri kwa siku 30. Akihutubia Taifa kutoka Ikulu, amesema baa zitaendelea kufungwa kwa siku 30 huku akiagiza Wizara ya Afya kukutana na wamiliki ili kupata muongozo sahihi wa kuzifungua. Aidha, Rais Kenyatta ameongeza idadi ya watu wanaoweza kuhudhuria misiba na harusi kutoka 15 iliyokuwepo awali hadi 100.Migahawa itafungwa saa 2 usiku baada...
Published 08/27/20
Mahakama imemhukumu kifungo cha maisha jela bila uwezekano wa msamaha Brenton Tarrant(29) aliyeua watu 51 kwenye misikiti miwili nchini humo.mtoto mwenye umri wa miaka 3 alikuwa miongoni mwa waliouawa. Machi mwaka jana, waumini waliokuwa wanasali katika msikiti wa Al Noor na Linwood walishambuliwa na Tarrant ambae alirusha tukio hilo mubashara Kupitia mtandao wa facebook. New Zealand haina adhabu ya kifo na Jaji Cameron Mander amesema hukumu hiyo hutolewa kwa wauaji wabaya zaidi,akiongezea...
Published 08/27/20
Mchezaji wa muda mrefu ndani ya klabu ya Valencia, Dani Pajero amejikuta akitokwa na machozi baada ya kupigwa chini na klabu yake ya Valencia, na sasa ataichezea klabu ya Villarreal ambao ni wapinzani wa Valencia. Kiungo huyo wa kati wa Uhispania amecheza Valencia mechi 383 tangu mwaka 2008 alipojiunga na klabu hiyo akitokea Getafe, na mwaka 2011 alikaririwa akisema kuwa ndoto yake ni kuja kustaafu klabuni Hapo, lakini kwa bahati mbaya ameshawekwa pembeni. Itakumbukwa Pajero alifanikiwa...
Published 08/15/20
Sampuli ya vipapatio / mabawa ya kuku yaliyogandishwa, zimegundulika kuwa na virusi vya Corona mjini Shenzhen. Nyama hizo ziliagizwa kutoka nchini Brazil. Baada ya ugunduzi huo, mamlaka za afya ziliwatafuta na kuwapima watu waliokuwa karibu na bidhaa hiyo ambapo majibu yamesema kuwa hawana maambukizi. Aidha eneo ambalo vipande vyenye virusi viliwekwa limepuliziwa dawa na mamlaka inatafuta bidhaa zingine za kampuni hiyo ambayo bado haijawekwa wazi. Hata hivyo shirika la Afya Duniani (WHO)...
Published 08/15/20
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Linah Sanga (Linah) ameamua kuuvunja ukimya baada ya kusambaa taarifa za kuwepo na mahusiano ya kimapenzi kati yake na mchezaji wa Simba, Benard Morrison. Ule msemo wa "uongo ukiachwa ukasambaa kwa ukubwa zaidi, huwa unageuka ukweli" umejaribu kupingwa vikali na mrembo huyo na kusema kuwa, Yeye na Benard Morrison Ni washkaj tu na wala hakuna mapenzi yoyote yanayoendelea kati yao kama watu wanavyodhani. Linah akaongezea kwa kusema, "yeye ni shabiki yake na...
Published 08/15/20
Rais wa Iran Hassan Rouhani ametishia kuwepo na madhara iwapo baraza la usalama la umoja wa Mataifa litarefusha marufuku ya silaha dhidi ya Iran kwa shinikizo la Marekani. Rouhani amesema kupitia televisheni ya taifa, kwamba azimio nambari 2231 la umoja wa Mataifa, ambalo ni sehemu ya makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa mjini Vienna mwaka 2015 linahitaji marufuku hiyo iondolewe ifikapo mwezi Oktoba. "Hivi sasa wamarekani wamependekeza azimio dhidi ya sehemu ya azimio nambari 2231 ili...
Published 08/13/20
Usaliti ni jambo baya sana katika mahusiano, usaliti si ujanja japo wengi wanaowaza kusaliti huwa wanajiona wajanja.wanajiona wamefanikiwa pale ambapo wanasaliti wenza wao kutogundua kama wanasalitiwa. Siku zote anaekusaliti huwa anajiona mjanja sana, kwamba yeye anasaliti mwenza wake hasaliti. Kwa asilimia kubwa wanaume hujiona kama usaliti ni halali yao, wanataka wao wasaliti lakini wapenzi nb wao wasithubutu kuwasaliti. Kwanini hawataki wenza wao wasaliti? eti wanaumia, hakuna kitu...
Published 08/13/20
1. Uhuru wa kifedha. Uhuru wa kifedha ni zaidi ya kuwa na fedha, uhuru wa kifedha ni kuwa mtu ambaye unatakiwa kuwa maishani na kuweza kufanya au kupata kile unachokihitaji maishani. Hata hivyo pesa ni muhimu sana kwenye suala la uhuru wa kifedha,ingawa pesa hizi zinatakiwa ziambatane na fikra sahihi. Kwa njia ya kujiwekea akiba utaweza kujijengea msingi mzuri wa kifedha ambao ukiambatanishwa na fikra sahihi utakuletea uhuru wa kifedha. 2. Matumizi mazuri ya pesa. Kama nilivyoeleza hapo...
Published 08/12/20
Mwinyi zahera ametambulishwa rasmi kuwa kocha Mkuu wa klabu ya Gwambina FC ambayo imepanda daraja msimu wa 2019/20 na itashiriki ligi kuu Bara msimu wa 2020/21. Zahera aliwahi kuifundisha yanga ndani ya ligi msimu wa 2018/19 na alianza nayo msimu wa 2019/20 kabla ya kufungashiwa virago kwa kile kilichoelezwa kuwa aliboronga kwenye michuano ya kimataifa. Kocha huyo amesaini dili la miaka 5 na inaelezwa kuwa ataanza kusajili nyota wake ambao alifanya nao kazi ndani ya Yanga. Wanaotajwa...
Published 08/11/20
Mamlaka ya Somalia inasema watu 10 wamefariki wakati wa majibizano ya risasi nje ya gereza la Mogadishu. Msemaji wa wizara ya habari alisema mahabusu 6 ambao walikuwa wanamgambo wa kundi la kigaidi Al-Shabab waliuliwa na askari wanne pia waliuawa. Chanzo cha majibizano ya risasi ni jaribio la mahabusu mmoja kutaka kutoroka. Kuna taarifa zinazosema mahabusu mmoja aliweza kupora bunduki kutoka kwa msimamizi wa gereza na baadae mahabusu na wafungwa wengine walivunja chumba cha kuhifadhia...
Published 08/11/20