UHUSIANO ULIOPO KATI YA KAZI NA WITO.
Description
Haijalishi uko wapi, unaishi wapi, wewe ni nani na unafanya nini. Ila ukweli ni kuwa kila mmoja wetu ana masaa 24 kwa siku. Na katika masaa hayo hayo tunatumia kwa kupumzika na kufanya mambo mbalimbali katika maisha.
Moja kati ya maswali mwanadamu amekua akijiuliza mara kwa mara, ni kutaka kufahamu dhumuni la maisha yake hapa duniani.
Tumekua tukijiuliza mimi ni nani? kwanini nipo hapa duniani?.Na katika kutafakari huko ndipo wengi wetu tunafikiria kuhusu kazi au wito wetu.
Kwani kuna utofauti mkubwa uliopo kati ya KAZI na WITO.
1. KAZI.
Neno "KAZI" linawakilisha aina ya huduma unayoitoa kwa mabadilishano. Kwa kufanya kazi unakua unatoa muda wako, juhudi, ujuzi, umakini, maarifa na ufahamu wako kwaajili ya kujipatia kipato.
Na kitendo hiki ndo kinajulikana kama AJIRA, BIASHARA, POSHO. Unaweza kuwa na sababu nyingi za kwanini kila siku unaenda kufanya kazi. Lakini kama haupo huru kifedha , kujiingizia kipato ndio azimio kuu la kazi.
2. WITO.
Neno "WITO" linawakilisha maslahi ya mtu binafsi, kile anachopenda, kinachomvutia na kumsukuma mtu. Wito sio kitu unachohitaji kukifanya, hiki ni kitu chenye msukumo mkubwa ndani yako.
Lakini licha ya hivyo wito unaweza kukuingizia kipato au ikawa kazi pia wakati huohuo. Wito unaweza kuja Kupitia njia mbalimbali mfano Sanaa, Usafi, au shughuli zozote za kibunifu (mfano Uandishi au uchoraji).
Lakini licha ya hivyo WITO wa kweli na wenye nguvu ni ule wa kiutumishi. Na kupitia wito huu ndipo utakutana na huduma kadhaa za kujitolea mfano kufundisha, kufanya kazi kwa pamoja, kutoa misaada mbalimbali.
Hapo ndio utajua utofauti wa KAZI na WITO.
KAZI : ni kwaajili ya kipato.
WITO : ni kwaajili ya utoshelezi.
Lakini inaweza kutokea unaipenda sana kazi yako mpaka upo tayari kufanya hata bure, basi hapo hubalika na kuwa WITO na sio KAZI. na ikiwa wito itaanza kuzalisha faida.