SIRI ZA MAFANIKIO YA MTU BINAFSI.
Listen now
Description
Neno mafanikio kila mtu huwa ana maana yake kwa wakati wake na kwa eneo lake katika maisha. Nikiwa na maana kuwa kila mtu ana tafsiri yake kuhusu mafanikio kutokana na muda na wakati alionao na anaoendelea kuishi hapa duniani. Mfano : kuna mafanikio ya kiafya, kiuchumi, kiuchumi, kimahusiano. Sasa katika makala yetu leo hii tutazungumzia zaidi juu ya Mafanikio ya kiuchumi na kifedha. Hizi ni Siri muhimu ambazo ni nguzo kuu za kukusaidia kufikia Mada makubwa kiuchumi na kifedha. 1. IMANI NA IBADA. Siku zote hakuna njia ya kufanikiwa kirahisi bila ya kuwa na imani na kufanya ibada, na ndio maana kuna watu wanashinda kwenye nyumba za ibada wakimuomba Mungu huku wengine wakikesha kwa waganga kutokana na imani yao ili kupata utajiri na mali. Lakini nikwambie tu MFANIKIO ya kweli na yenye furaha ni yale utakayoyapata kutokana na kumuamini mwenyezi Mungu pekee. Jifunze kufanya ibada kila mara na utambue kuwa binadamu sio kazi ya mikono yake pekee bali ni kazi inayotokana na Mungu pekee na kila binadamu ana fungu lake jema mbele ya mwenyezi Mungu aliye muumba. 2. KUFANYA KAZI KWA BIDII. Suala zima la kufanikiwa katika maisha linahitaji kujitoa kila mara na kufanya kazi kwa bidii hasa. Kwani kufanya kazi kwa bidii huendana na ufanisi na ujuzi wako ulionao. Acha kuwa mtu wa kulalamika sana na kukata tamaa mapema, bali anza sasa kujituma utaona mafanikio mapema sana. 3. KUWA MSOMAJI ZAIDI. Kusoma mambo mbalimbali yanayohusu maisha au kile kitu ulichowekeza katika maisha yako kukifanya, hiyo ni sehemu tosha inayoweza kukubadilisha fikra zako na kukufanya kuwa bora na kuwa mtaalamu au mfanisi mkubwa katika utafutaji wa mafanikio yako. Kusoma sio mpaka urudi darasani, ila nina maana kuwa UJIFUNZE kusoma hata mambo hata yale ya kawaida yanayohusu maisha na mafanikio binafsi. Anza kusoma vitabu mbalimbali vinavyohusu maendeleo ya mtu binafsi, utajiri, kuwekeza, afya, usafi, ufanisi wa kazi au masoko. Mfano vitabu kama Rich Dad poor Dad, Maximum Achievement, The power of positive thinking au Self Billionaire. 4. MAHUSIANO MZURI NA WATU. Kuwa na mahusiano na watu wako wa karibu ni jambo jema linaloweza kukuweka katika mazingira mazuri zaidi ya mafanikio makubwa na ukawa mtu wa tofauti na wengine katika nyanja za maisha. Kama usipokua na mahusiano mazuri na watu basi swala la kukosa furaha na amani kwako itakua ni la kawaida sana. 5. KUWA NA NIDHAMU YA MUDA. Muda ndio msingi mzuri na wa kipekee wa kukusaidia kufikia malengo yako uliyojiwekea. Huwezi kufikia mafanikio makubwa kama bado hauna nidhamu kwenye swala la muda. Jifunze kwenda na muda ili uongeze ubora katika kazi yako, heshima yako na nidhamu yako binafsi. 6. NIDHAMU YA MATUMIZI YA FEDHA. Ukishindwa kutumia fedha zako vizuri na kujiwekea akiba basi hesabu kuwa wewe utakuwa unafanya jambo ambalo halina mwisho wake. Kutokua na nidhamu ya fedha ni kama vile unataka kuanzisha safari bila kujua mwisho wake ni nini. 7. KUJIAMINI NA KUJIKUBALI BINAFSI. Kujiamini ni hali pekee ndani ya mtu ya kuwa jasiri bila uongo katika jambo lolote lile analolikabili mbele yake. Ukijiamini na kujikubali wewe mwenyewe itakua ni rahisi na wengine kukuamini.
More Episodes
Mziki mzuri na maelezo ya wasani mbalimbali yana patikana hapahapa jamsingi subscribe ili uwe wa kwanza kupata vibes connection
Published 11/16/20
Published 11/16/20
"COUNTRY BOY" AZUNGUMZIA UMUHIMU WA MSANII KUWA TRENDING YOUTUBE NA VIEWS WENGI KWENYE MUZIKI WAKE.
Published 11/10/20