KENYA: MUDA WA WANANCHI KUTOTOKA NDANI WAONGEZWA KWA SIKU 30.
Description
Katika jitihada za kudhibiti maambukizi ya Covid-19, Rais Uhuru Kenyatta ameongeza muda wa wananchi kutotoka ndani kuanzia saa 3 usiku hadi saa 10 alfajiri kwa siku 30.
Akihutubia Taifa kutoka Ikulu, amesema baa zitaendelea kufungwa kwa siku 30 huku akiagiza Wizara ya Afya kukutana na wamiliki ili kupata muongozo sahihi wa kuzifungua.
Aidha, Rais Kenyatta ameongeza idadi ya watu wanaoweza kuhudhuria misiba na harusi kutoka 15 iliyokuwepo awali hadi 100.Migahawa itafungwa saa 2 usiku baada ya saa 1 usiku kuanzia kesho.
Pia, Rais amezitaka Wizara za michezo na Afya kuandaa miongozo ya pamoja ili kurejesha shughuli za michezo nchini humo.
Kama utakumbuka siku mbili zilizopita ndani ya Taifa hilo kulikuwa na taarifa za madarasa ya shule binafsi kwasasa yanatumiwa kufugia kuku kutokana na shule kufungwa mpaka mwezi Januari, 2021.
Kenya imerekodi visa 33,016 na vifo 564 huku idadi ya wagonjwa waliopona ikiwa 19,296.