Episodes
Mfanyabiashara,Tariq Machibya (29) maarufu kama Mr kuku, amefikishwa mahakama ya kisutu, akikabiliwa na mashtaka 7 likiwemo la kufanya biashara haramu ya upatu kwa kukusanya fedha za umma zaidi ya Tsh. bilioni 17.
Machibya amesomewa mashitaka yake tarehe 10.08.2020 na wakili mwandamizi wa Jamhuri, Simon Wankyo mbele ya hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Godfrey Isaya.
Mbali na shtaka la kusimamia biashara haramu ya upatu,Mr kuku anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi pia ana mashtaka ya...
Published 08/11/20
Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani amesema atatoa amri ya kuachiwa huru kwa wafungwa 400 wa kundi la wanamgambo wa Taliban baada ya baraza la jadi la viongozi wa kikabila kuunga mkono hatua hiyo kama njia ya kufufua mazungumzo ya amani.
Akizungumza wakati wa hotuba yake ya kufunga mkutano wa baraza hilo linalojulikana kama 'loya jirga' amesema atatia saini amri hiyo kama ilivyotakiwa na kundi la Taliban na baada ya viongozi hao wa kikabila kufikia mwafaka.
Uamuzi huo utaondoa kikwazo cha...
Published 08/10/20
Tarehe 09, Agosti, Malawi imetangaza kuyafunga makanisa yote na kumbi za starehe katika awamu mpya ya vizuizi vya kudhibiti ongezeko linalotia wasiwasi la Virusi vya Corona.
Vizuizi vipya vilivyotangazwa Kupitia gazeti la serikali vinajumuisha pia amri ya kuvaa barakoa na marufuku kwa Mikusanyiko inayozidi watu 10 isipokuwa kwa shughuli za mazishi zitakazo ruhusu jumla ya watu 50.
Mwanasheria Mkuu wa serikali Chikosa Silungwe, amesema kikosi maalumu cha maafisa wa jeshi kimeundwa...
Published 08/10/20
Washindi wa soka la FA Arsenal wana mlenga beki wa kati wa Brazil Diego Carlos huku Mikel Arteta akipanga marekebisho makubwa msimu ujao.(Telegraph - Subscription required).
Arsenal itatoa ofa kwa mshambuliaji wa Gabon Pierre -Emerick Aubameyang,31,wiki hii ya pauni milioni 250,000 kwa wiki katika makubaliano ya miaka mitatu kuendelea kusalia kwenye klabu hiyo.(mirror)
Hata hivyo, Aubameyang anataka Arsenal kutia saini makubaliano ya hali ya juu kabla ya kukubali mkataba mpya baada ya...
Published 08/04/20
Mkuu wa zamani wa kanisa katoliki, Papa Benedict XVl,ameripotiwa kuumwa sana baada ya kumtembelea kaka yake aliyekuwa mgonjwa nchini Ujerumani na sasa hali yake ni dhaifu sana.
Gazeti la Pasaauer Neue presse la nchini Ujerumani limeripoti kwamba Papa Benedict Mwenye umri wa miaka 93 anasumbuliwa na Ugonjwa unaotokana na kirusi kinachosababisha pelepele usoni na maumivu makali, kwa muujibu wa mwandishi wa tawasifu ya Papa huyo , Peter Seewald.
Kwa muujibu wa Seewald,"Papa kwa sasa ana hali...
Published 08/04/20
Katika harakati zako za kutafuta mpenzi, unaweza kukutana na mwanamke ambaye kwasababu moja ama nyingine anakuondolea uwezo wako wa kufikiri, kutumia mantiki na pia kutumia akili yako ya kuzaliwa.si lazima awe amekufanyia kitu, lakini inaweza kuwa ni ulevi wako tu unasababisha ufanye mambo yasiyo ya kawaida.pengine ndio maana baadhi ya wasanii huzungumzia suala la "kudata" kutokana na mapenzi.
Ni jambo jema kudhani kuwa wewe na mpenzi wako mnapendana kwa dhati na kwamba kila mmoja amefika...
Published 08/04/20
Mahakama ya Somalia imemuhukumu mwandishi wa habari maarufu nchini humo, Abdiaziz Ahmed Gurbiye kifungo cha miezi 6.
Abdiaziz ambae ni mhariri mkuu na naibu mkurugenzi wa shirika binafsi la Goobjoog, mjini Mogadishu, alishtakiwa kwa kuikosoa Serikali ya Somalia katika kukabiliana na mlipuko wa Corona.
Mahakama ya mjini Banadir ilimtaka kutoa faini ya shilingi milioni 5 za Somalia (208.3 USD) kwa kuchapisha taarifa za kizushi na kuitusi Serikali na mahakama, muda mfupi baada ya kuhamishiwa...
Published 07/30/20
Rais wa Rwanda Paul Kagame ametangaza siku 3 za maombolezo kuanzia July 27 - 29, 2020 kufuatia kifo cha aliekuwa Rais wa Tanzania, Benjamin William Mkapa.
Kagame ambae pia ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika mashariki (EAC) amemzungumzia Hayati Benjamin kama kiongozi ambae mchango wake ulienda nje ya mipaka ya Tanzania.
Vilevile Serikali ya Burundi imetangaza siku 3 za maombolezo kutokana na kifo cha Benjamin William Mkapa.
Waziri mkuu wa Burundi, Alain Guillaume Bunyoni atakaeiwakilisha...
Published 07/27/20
Viongozi wa Mataifa ya Afrika magharibi wamemaliza siku nzima wa mkutano wa kilele hapo tarehe 24, Julai bila ya kufukia makubaliano juu ya mgogoro wa kisiasa unaotokota nchini Mali.
Viongozi watano wa Mataifa ya Afrika magharibi wamekutana na Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita, pamoja na viongozi wa vuguvugu la maandamo wanaomtaka ajiuzulu.
Hata hivyo, upatanishi ilishindikana,na Rais wa Niger Mahamadou Issoufou pamoja na wenzake wa Senegal,Ivory Coast, Ghana, Nigeria wamesema jumuiya ya...
Published 07/26/20
Wizara ya mambo ya nje ya China,imeiamuru Marekani kufunga jengo lake la kidiplomasia lililopo Chengdu China, Uamuzi umekuja baada ya Marekani kufunga ofisi ya kidiplomasia ya China iliyopo Texas, Marekani.
Kufungiana ofisi za kidiplomasia linaonekana kuwa suala linalozidi kuleta utengano kwa Mataifa hayo ambayo awali yalianza kwa kuwekeana vikwazo katika upatikanaji wa VISA,na kuongeza sheria kwa wanaosafiri kidiplomasia.
Awali, Marekani ililaumu ofisi za China wanasaidia wizi wa kijeshi...
Published 07/26/20
Idadi ya watu wanaotafuta hifadhi nchini Ujerumani kutokutoka na vita ama mateso katika nchi zao iliongezeka kupita milioni 1.8 mwishoni mwa mwaka jana kulingana na takwimu rasmi zilizotolewa tarehe 23, Julai.
Idara ya takwimu ya serikali kuu (Destatis) imesema kuwa nb idadi hiyo iliongezeka kwa kiwango cha chini cha kila mwaka kutoka asilimia 3 mnamo mwaka 2012, idadi hiyo ilijumuisha raia wa kigeni ambao walikuja nchini Ujerumani kwasababu za kisheria, kisiasa ama kibinadamu.
Mnamo...
Published 07/25/20
Miili ya watu 7 imegunduliwa katika kaburi moja katika mji uliokuwa umetekwa na waasi Libya.
Miili ya watu 7 ambao wanakisiwa kuwa raia imegunduliwa katika mji wa Terhune, mji ambao ulikuwa umetekwa na waasi nchini Libya.
Mji huo ulikombolewa mnamo June 5 baada ya makubaliano makali kati ya jeshi la serikali inayotambulika na jumuiya ya kimataifa na wapiganaji wa jenerali Khalifa Haftar.
Kiongozi wa jopo lililoandaliwa kwa ajili ya kufanya uchunguzi kuhusu mauaji katika maeneo yaliyokuwa...
Published 07/25/20
Jaji mkuu wa Iran Ebrahim Rais amefifisha matumaini kwamba adhabu ya kifo iliyotolewa kwa waandamanaji watatu vijana wa kiiran itafutwa kufuatia malalamiko ya mitandaoni.
Jaji mkuu huyo amesema maandamano yanakubalika lakini machafuko na fujo vinavyohatarisha usalama wa taifa ni mstari mwekundu.
Ameongeza katika matamshi yaliyochapishwa na shirika la habari Isna, kwamba katika matukio kama hayo mahakama haiwezi kushawishiwa na kampeni na propaganda.
Chini ya hashtag ya kupinga hukumu hiyo...
Published 07/22/20
Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch,limedai kuwa kuna Utamaduni wa udhalilishaji wa kimwili wa kimaneno unaowalenga wanariadha vijana nchini Japan,Ikiwa imesalia mwaka mmoja kuelekea mashindano ya michezo ya olimpiki ya dunia yanayopangwa kufanyika mjini Tokyo.
Shirika hilo limesema lilifanya mahojiano zaidi ya 50 na wanariadha watoto wa sasa na wa zamani kwa ngazi tofauti za mashindano, utafiti wa mtandaoni na mashirika ya michezo.
Waligundua kuwa watoto nchini...
Published 07/22/20
1. Inachangia kufahamika zaidi kwa biashara yako.
Mitandao ya kijamii ni moja ya njia za kutangaza biashara yako kwa gharama nafuu zaidi na inauhakika wa kuwafikia wateja wengi zaidi, kwani asilimia kubwa ya watu wengi sasa hivi wanatumia muda mwingi sana katika mitandao ya kijamii hivyo kutangaza biashara yako kutakuongezea idadi ya wateja na watu wenye ufahamu wa kutosha kuhusu biashara yako kwa ujumla.
2. Inapanua wigo wa kupata wateja wapya tofauti na wale wanaokuzunguka.
Kutumia...
Published 07/21/20
Naomba pasipo kupoteza wakati nikukaribishe katika somo letu la leo,na siku ya leo tutazungumza kuhusiana na mbinu moja itakayo kusaidia katika ukuaji wa biashara.
Moja kati ya changamoto kubwa kubwa ya ufanyaji wa biashara ni kule kufanya kazi kwa mazoea, nasema hivi kwasababu wafanyabishara wengi husikika wakisema ya kwamba mteja ni mfalme, lakini katika hili kumekuwa na ukakasi ni wateja wachache sana ambao huona ufalme huo.
Hii ni kwasababu wafanyabishara wachache sana ambao wamekuwa...
Published 07/21/20
Wakati taifa la Tanzania likiwa kwenye maandalizi ya uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu 2020, huku ikishuhudiwa muamko mkubwa wa wasanii na watu maarufu wakijitokeza kuchukua fomu kwaajili ya kuhitaji ridhaa ya kugombea nafasi mbalimbali. Nchini Marekani msanii Kanye West amejitoa kwenye mbio hizo za kugombea nafasi ya Urais.
Rapa Kanye West alitangaza azma yake ya kugombea nafasi ya Urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu ndani ya Marekani, huku akiwa anajaribu kushindana na Donald Trump...
Published 07/15/20
Uingereza imepiga marufuku Kampuni ya Huawei kuweka mitambo ya 5G huku kampuni kama BT (BTGOF) na Vodafone (VOD) zikipewa muda mpaka 2027 kuondoa mitambo ya kampuni hiyo kwenye mitandao yao.
Waziri wa masuala ya kidigitali na Utamaduni, Oliver Dowden amesema kutokana na hali ya sintofahamu inayozunguka Kampuni hiyo ya china, Uingereza imekosa imani na mitambo ya 5G ya Huawei.
Marufuku iliyotolewa na Uingereza ni ushindi mkubwa kwa Marekani ambayo imekua ikishinikiza Mataifa kupiga marufuku...
Published 07/15/20
Hayo yameelezwa na mwanamuziki Diamond Platinumz Wakati lebo ya WCB ikizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Kuhusu usiku wa Zuchu utakaokuwa Julai 18 mwaka huu mlimani city jijini Dar es salaam.
"Sijui kama nilitakiwa kusema hili au la, lakini bosi wangu Sallam atakuwa balozi wa Universal Music Group east Afrika (Afrika mashariki),na tunaamini kupitia yeye ataboresha zaidi", ametangaza Diamond.
Mwanamuziki huyo amesema hayo wakati akijibu swali la mwandishi wa habari...
Published 07/14/20
Ule msemo wa wapendanao wakigombana chukua jembe ukalime, umeonekana kudhihirika baada ya Princess Love ambae ni mke wa msanii Ray J, kuamua kurudi mahakamani kusitisha kesi yake ya kudai talaka kutoka kwa mumewe.
Princess Love alifungua file la kudai talaka mwanzoni mwa May, 2020 Baada ya kuwa Kwenye mahusiano ya ndoa na Ray J kwa kipindi cha miaka 4, huku wakifanikiwa kupata watoto wawili (Melody love & Epik Ray).
Wawili hao wamekuwa hawaishi pamoja kwa muda wa mwaka mmoja sasa, huku...
Published 07/14/20
.Habari rafiki mpendwa, natumaini unaendelea vizuri na mapambano ya maisha.Nikutie tu moyo endelea na harakati hizo naamini ipo siku utayaona matunda ya unachokifanya.Kama kawaida leo nakuletea makala nyingine hii ni juu ya sifa za mjasiriamali.
Kuna watu wengi sana wanajiita wajasiriamali lakini kiuhalisia si wajasiriamali.Hii imenifanya nifikirie juu ya hili.
Zifuatazo ni sifa za mjasiriamali na kama huna sifa kati ya hizi basi hujawa mjasiriamali wa ukweli bali utakuwa unabip tu.
sifa...
Published 07/14/20
Zifuatazo ndizo hatua tano jinsi ya kuwa mfanyabiashara mwenye mafanikio.
1. Ainisha aina za biashara ambazo unataka kuzifanya.
katika hili ni kwamba kama unataka kuwa mfanyabiashara mwenye mafanikio, unatakiwa kuainisha aina mbalimbali za biashara ambazo unataka kuzifanya huwenda zikawa ni zaidi ya biashara hata sita.Ukisha pata biashara hizo jaribu kuwashirikisha hata baadhi ya ndugu na jamaa ili wakupe mtazamo wao ni biashara ipi inafaa.
2. Chagua biashara moja ambayo unaona...
Published 07/13/20
Mwanamuziki wa bongo na mfanyabiashara Shilole ameibuka tena baada ya siku chache kuposti picha zikimuonyesha ameumizwa na mume wake baada ya kupigwa na mumewe leo ameibuka na kuwashukuru watanzania kwa ushirikiano Kipindi cha matatizo yake.
Kupitia ukurasa wake wa instagram Shilole aliandika hivi
Salaam ndugu zangu,
Nimeona upendo, nimeona heshima na kukubalika kwa kiwango cha pekee katika wakati huu wa changamoto niliyokutana nayo.
Nashukuru sana kwa upendo wenu, nashukuru sana wote...
Published 07/13/20
Luteni Jenerali Madeline Swegle amekuwa mwanamke wa kwanza Mmarekani mweusi kuendesha ndege ya kivita inayotumiwa na kikosi cha wanamaji cha Marekani.
Ameandika historia kwa kupaa angani kama rubani wa ndege ya kivita ya Marekani inayotumiwa na wanamaji na atatunukiwa cheo cha "wings of Gold" au (mbawa za dhahabu), baadae mwezi huu wa Julai kwa mujibu wa ujumbe wa twitter uliotumwa alhamisi wiki hii na mkuu wa mafunzo ya ndege za kijeshi za majini.
Mkuu wa mafunzo ya kijeshi alimsifu Bi...
Published 07/13/20
Diamond na Alikiba pamoja na wasani wengine kutumbwiza pamoja na kwenye jukwa moja hukwo DODOMA
Published 07/13/20