KANYE WEST AJITOA KWENYE MBIO ZA KUGOMBEA URAIS WA MAREKANI.
Description
Wakati taifa la Tanzania likiwa kwenye maandalizi ya uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu 2020, huku ikishuhudiwa muamko mkubwa wa wasanii na watu maarufu wakijitokeza kuchukua fomu kwaajili ya kuhitaji ridhaa ya kugombea nafasi mbalimbali. Nchini Marekani msanii Kanye West amejitoa kwenye mbio hizo za kugombea nafasi ya Urais.
Rapa Kanye West alitangaza azma yake ya kugombea nafasi ya Urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu ndani ya Marekani, huku akiwa anajaribu kushindana na Donald Trump ambae alikua ni rafiki yake kwenye harakati za kumsaidia kumfanyia kampeni wakati anataka kuingia White House.
Taarifa za Kanye West kujiondoa kwenye mbio hizo zimetolewa na watu wa karibu sana ambao walikuwa kwenye kamati yake ya kampeni.
Taarifa zinasema timu ya Kanye West tayari ilikuwa imeshaingia kwenye majimbo ya Florida na Carolina Kwaajili ya kuanza kuwaandaa baadhi ya wanahabari ili kujitengenezea mazingira mazuri kwenye kampeni yao, jambo ambalo lilihitaji mawakili wengi kushiriki na kuliunga mkono.
Kwenye taarifa hiyo, wanasema watu wengi walijitokeza kumuunga mkono rapa Kanye West na kusaini, namba ilikua kubwa mpaka ikatuzidi huku watu wengi waliamua sio tu kusimamia mikataba yao lakini walijitolea pia.
Lakini baadae kidogo baada ya chanzo hicho kuulizwa kuhusu maendeleo ya timu ya kampeni ya Kanye, Jibu lilikua ni "Amejitoa" Pindi alipoulizwa zaidi kuhusu mwisho wa mbio za kugombea urais za Kanye West akajibu "Nitawafahamisha ninachojua mara moja"