VIONGOZI WA AFRIKA WASHINDWA KUPATANISHA MZOZO WA MALI.
Description
Viongozi wa Mataifa ya Afrika magharibi wamemaliza siku nzima wa mkutano wa kilele hapo tarehe 24, Julai bila ya kufukia makubaliano juu ya mgogoro wa kisiasa unaotokota nchini Mali.
Viongozi watano wa Mataifa ya Afrika magharibi wamekutana na Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita, pamoja na viongozi wa vuguvugu la maandamo wanaomtaka ajiuzulu.
Hata hivyo, upatanishi ilishindikana,na Rais wa Niger Mahamadou Issoufou pamoja na wenzake wa Senegal,Ivory Coast, Ghana, Nigeria wamesema jumuiya ya uchumi wa Mataifa ya Afrika magharibi, ECOWAS itaitisha mkutano mwingine wa kilele Jumatatu.
Vuguvugu la Juni 5 lililopewa jina la siku yalipoanza maandamo hayo,linamtaka Keita aondoke madarakani kwa kushindwa kushughulikia uliyoporomoka nchini humo ufisadi pamoja na uasi wa miaka minne wa makundi ya kijihadi.