FAIDA ZA KUTUMIA MITANDAONI YA KIJAMII ILI KUTANGAZA BIASHARA YAKO.
Description
1. Inachangia kufahamika zaidi kwa biashara yako.
Mitandao ya kijamii ni moja ya njia za kutangaza biashara yako kwa gharama nafuu zaidi na inauhakika wa kuwafikia wateja wengi zaidi, kwani asilimia kubwa ya watu wengi sasa hivi wanatumia muda mwingi sana katika mitandao ya kijamii hivyo kutangaza biashara yako kutakuongezea idadi ya wateja na watu wenye ufahamu wa kutosha kuhusu biashara yako kwa ujumla.
2. Inapanua wigo wa kupata wateja wapya tofauti na wale wanaokuzunguka.
Kutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya kutangaza biashara yako kuna kuongezea wigo wa wateja wapya ambao ni vigumu kufahamu kuhusu biashara yako kwani wako mbali na eneo la biashara husika lakini Mitandaoni ya kijamii inakupatia nafasi ya watu wote watakao Kutana na tangazo la biashara yako kuifahamu na kushawishika kutumia bidhaa zako na hivyo kugeuka wateja wa biashara yako.
3. Inajenga uhusiano wa karibu na wateja wako.
Kupitia ukaribu unaojengeka baina ya biashara yako na wateja wako hii inasaidia kuweka ukaribu wa kusikiliza maoni, shida na kutafuta ufumbuzi kiurahisi wa kero za wateja wako kwani kwa urahisi kabisa wanaweza kuwasilisha maoni yao kupitia akaunti za biashara yako za mitandao ya kijamii.
4. Inaongeza imani na uaminifu wa watu kwenye biashara yako.
Moja ya malengo ya kila biashara ni kutengeneza wateja waaminifu na wakudumu wa bidhaa za biashara hiyo, hivyo Mitandaoni ya kijamii kupitia ukaribu unaojengeka baina ya biashara na wateja wake na urahisi wa taarifa za biashara yako kumfikia mteja inapeleka kutengeneza wateja waaminifu na wakudumu wa biashara yako.
5. Inasaidia kupunguza gharama za uendeshaji wa biashara yako.
Biashara nyingi hutumia fedha nyingi kwaajili ya kujitangaza na hili huonekana pale ambapo njia zinazotumika kutangaza biashara husika zinakuwa ni ghali sana na hivyo kuongeza gharama za uendeshaji wa biashara husika. Kupitia matumizi ya mitandao ya kijamii kama njia ya kujitangaza inapunguza gharama hizo na kujitangaza na kupelekea kupunguza gharama za uendeshaji wa biashara na kuipatia nafasi nzuri ya kifedha zaidi.
6. Inaongeza ufahamu wa kutosha dhidi ya soko husika na wateja wako.
Kupitia ukaribu unaojengeka wateja wako katika mitandao ya kijamii na kujibu comments za wateja wako katika mitandao ya kijamii hii inapelekea biashara husika kupata taarifa za kutosha za soko husika na kuipa nafasi biashara kuwa na taarifa za kutosha za wateja wake na hii inasaidia biashara Kufanya maamuzi na kuweka mikakati inayohitajika kwa wakati husika na soko husika.
Hizo ni baadhi ya faida za kuitumia mitandao ya kijamii kuitangaza biashara yako na kama bado haujaanza kutumia mitandao ya kijamii ni vyema ukaanza sasa kwani unapitwa na mengi ambayo biashara yako ingenufaika kwa kutumia mitandao ya kijamii.
Asilimia 90 ya wataalamu wa masoko wanakiri kuwa Mitandaoni ya kijamii ina nguvu sana katika kutangaza biashara na imekuwa ikionyesha matokeo chanya katika biashara zao.baadhi ya mitandao ya kijamii inayotumika sana katika matangazo ya biashara ni kama Facebook, Instagram, Twitter, Blogs, YouTube, LinkedIn,nk.