Description
Mwanamuziki wa bongo na mfanyabiashara Shilole ameibuka tena baada ya siku chache kuposti picha zikimuonyesha ameumizwa na mume wake baada ya kupigwa na mumewe leo ameibuka na kuwashukuru watanzania kwa ushirikiano Kipindi cha matatizo yake.
Kupitia ukurasa wake wa instagram Shilole aliandika hivi
Salaam ndugu zangu,
Nimeona upendo, nimeona heshima na kukubalika kwa kiwango cha pekee katika wakati huu wa changamoto niliyokutana nayo.
Nashukuru sana kwa upendo wenu, nashukuru sana wote walionijulia hali na kuniombea dua.
Kuhusu maendeleo yangu mimi niko sawa naendelea kupambana.Changamoto ni sehemu ya maisha haziwezi kunifanya nianguke, lakini yote hayo si kwa nguvu zangu ni Mungu pamoja na watanzania wenzangu mnaonitakia mema.
Maisha yanaendelea tuendelee kuijenga jamii yetu, jamii inayokataa unyanyasaji wa kijinsia.
Kutokana na yaliyomkuta Shilole naamini kabisa bado katika jamii zetu mambo haya yapo na yanawakuta wanawake wengi hasa sehemu za vijijini kutokana na kwamba bado kuna mambo ya unyanyasaji wa kijinsia.
Taarifa ya Shilole natumaini itakuwa imewagusa wengi ambao wanakutana na changamoto kama hizi na waweza kuamka na kuzipinga kwa kutoa taarifa sehemu husika ili wanaofanya vitendo hivi vya unyanyasaji wa kijinsia vifike kikomo na tuishi kwa amani katika jamii zetu.