HUMAN RIGHTS WATCH YAIKOSOA JAPAN KWA UDHALILISHAJI WATOTO KATIKA MAANDALIZI YA OLIMPIKI.
Description
Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch,limedai kuwa kuna Utamaduni wa udhalilishaji wa kimwili wa kimaneno unaowalenga wanariadha vijana nchini Japan,Ikiwa imesalia mwaka mmoja kuelekea mashindano ya michezo ya olimpiki ya dunia yanayopangwa kufanyika mjini Tokyo.
Shirika hilo limesema lilifanya mahojiano zaidi ya 50 na wanariadha watoto wa sasa na wa zamani kwa ngazi tofauti za mashindano, utafiti wa mtandaoni na mashirika ya michezo.
Waligundua kuwa watoto nchini Japan,bado wanapitia udhalilishaji michezoni na limeainisha maswala ya kitaasisi ambayo yanayofanya uitikiaji wa taifa hilo kwa matukio kama hayo kukosa ufanisi.
Shirika la michezo la Japan limesema linafahamu Kuhusu ripoti hiyo na kuongezea kuwa limechukua hatua kuondoa udhalilishaji kwenye michezo, ikiwa ni pamoja na kuunda Mtaala wa mafunzo au kutengeneza miongozo kwa mashule.