MBINU MPYA ZA KUMFANYA MTEJA WAKO KUWA MFALME.
Description
Naomba pasipo kupoteza wakati nikukaribishe katika somo letu la leo,na siku ya leo tutazungumza kuhusiana na mbinu moja itakayo kusaidia katika ukuaji wa biashara.
Moja kati ya changamoto kubwa kubwa ya ufanyaji wa biashara ni kule kufanya kazi kwa mazoea, nasema hivi kwasababu wafanyabishara wengi husikika wakisema ya kwamba mteja ni mfalme, lakini katika hili kumekuwa na ukakasi ni wateja wachache sana ambao huona ufalme huo.
Hii ni kwasababu wafanyabishara wachache sana ambao wamekuwa wakijua ni nini maana ya mteja.
Wafanyabishara wengi wamekuwa wakimchukulia mteja pale anapokuja kwenye biashara ambayo anafanya tu.kufanya hivi kutakufanyanya kuiona ramani ya biashara haina usawa kwani biashara utazidi kuiona ni ngumu siku zote.
Hivyo ili uweze kumfanya mteja wako awe mfalme unatakiwa kufanya mambo yafuatayo;
1. Acha mara moja kumsubiri mteja wako aje kukufuata mfanyabiashara mahali ulipo, bali anza utaratibu wa kumfuata mteja wako mahali alipo, Kufanya hivyo kutamfanya mteja wako ajisikie huru na pia ajihisi kuwa yeye ni mfalme kweli na kufanya hivi kutamjengea utaratibu mpya na pia kujiona yeye si kama tu mteja bali ni sehemu ya biashara yako.
2. Tengeneza utaratibu mpya wa kuwa na mawasiliano ya karibu na mteja wako,si umekuwa ukisema ya kwamba mteja ni mfalme, kama ndivyo hivyo basi hakikisha ya kwamba unakuwa na mawasiliano na wateja, Mawasiliano hayo basi naomba yawe ni kwaajili ya biashara tuu na si vinginevyo na kama ukiyatumia mawasilaino hayo vibaya basi jiandae kuwapoteza wateja wako wote, Mawasiliano hayo yanatumika kuwajuza wateja wako kuhusu ujio wa bidhaa mpya na mambo mengine muhimu kuhusu biashara tu.
3. Jifunze mbinu mpya ya kuweza kufanya mazungumzo na wateja, hivi hujawahi enda katika biashara ya mtu mwingine mpaka ukajuta kwanini ulienda mahali hapo, bila shaka kama hali hii imewahi kukutokea basi ni vyema katika biashara yako uweze kujenga utaratibu mpya ambao utakufanya wateja wako wajisikie huru kila wakija kwako.
4. Uchawi mkubwa ambao unafanyika katika biashara ni kutoa ofa kwa wateja wako.
Hii siri ambayo nakuibia wewe siku ya leo, haijalishi ni biashara gani ambayo unaifanya ila ili uweze kukua katika biashara hiyo ni vyema ukajiwekea utaratibu wa kutoa ofa kama yafanyavyo makampuni ya simu Kufanya hivyo kutawafanya wateja wengi waje kwako.
Asante sana kwa kusoma makala haya, mpaka kufikia hapo sina la ziada nikutakie kazi njema na siku njema.