MBINU TANO ZA KUTAKA KUINGIA KATIKA BIASHARA.
Description
Zifuatazo ndizo hatua tano jinsi ya kuwa mfanyabiashara mwenye mafanikio.
1. Ainisha aina za biashara ambazo unataka kuzifanya.
katika hili ni kwamba kama unataka kuwa mfanyabiashara mwenye mafanikio, unatakiwa kuainisha aina mbalimbali za biashara ambazo unataka kuzifanya huwenda zikawa ni zaidi ya biashara hata sita.Ukisha pata biashara hizo jaribu kuwashirikisha hata baadhi ya ndugu na jamaa ili wakupe mtazamo wao ni biashara ipi inafaa.
2. Chagua biashara moja ambayo unaona inafaa.
Hatua ya pili baada ya kuwashirikisha ndugu na jamaa, unachotakiwa kufanya ni kwamba kaa chini pamoja na halmashauri yako ya kichwa ili kuweza kupambanua ni biashara ipi ambayo inafaa, baada ya kupata majibu tafakari kisha chagua mwenyewe biashara moja ambayo itakuwa na faida kwako hapo mbeleni.
3. Fanya utafiti juu ya washindani wako.
Baada ya kupata wazo moja la biashara hatua ya tatu ni kwamba unatakiwa kufanya utafiti wa juu ya washindani wako ambao tayari umewakuta wakifanya biashara.Na katika kufanya utafiti wako unatakiwa kujua ni mbinu zipi ambazo wao huzitumia katika kupata wateja, baada ya kujua hii itakusaidia kujua mbinu mpya ambayo itakufanya uweze kuwavuta baadhi ya wateja ili waje kwako.
4. Tengeneza mpango wa biashara hiyo.
Baada ya kujua mbinu za kuwatambua na kuwashinda washindani wako, jambo la nne ni kuhakikisha unaandaa mpango biashara ambao ndiyo utaongoza biashara yako.katika mpango wa biashara ndio ambao utakusaidia kwa kiwango kikubwa kujua biashara yako jinsi ambavyo utakavyokuwa.Nakusihi tuu endelea kufuatana nami afisa mipango kila wakati nitakueleza siku nyingine jinsi ya kuandaa mpango wa biashara.
5. Tafuta mtu atakaye kuongoza na kusimamia katika biashara yako.
Mwisho kabisa ili uweze kufanikiwa katika biashara yako unahitaji kuwa na mtu wa kuongoza katika biashara yako, mtu huyo anatakiwa kuwa mzoefu katika biashara ambayo unatakiwa kufanya.Uzoefu w mtu huyo litakuwa darasa tosha kwako na kukuelekeza ni nini ufanye na nini usifanye.
Lakini nikuibie siri moja, hatuna siri kubwa katika mafanikio makubwa ya kibiashara kama kuwa mbunifu, ubunifu ndio siri na silaha makini ya utendaji wako wa kibiashara yenye mafanikio.