PAPA BENEDICT WA 16 ANA HALI MBAYA.
Listen now
Description
Mkuu wa zamani wa kanisa katoliki, Papa Benedict XVl,ameripotiwa kuumwa sana baada ya kumtembelea kaka yake aliyekuwa mgonjwa nchini Ujerumani na sasa hali yake ni dhaifu sana. Gazeti la Pasaauer Neue presse la nchini Ujerumani limeripoti kwamba Papa Benedict Mwenye umri wa miaka 93 anasumbuliwa na Ugonjwa unaotokana na kirusi kinachosababisha pelepele usoni na maumivu makali, kwa muujibu wa mwandishi wa tawasifu ya Papa huyo , Peter Seewald. Kwa muujibu wa Seewald,"Papa kwa sasa ana hali dhaifu sana" limeandika gazeti hilo ."Akili na uwezo wake wa kufikiri bado viko makini lakini sauti yake inasikika kwa shida sana. Seewald alimtembelea Papa Benedict mjini Rome siku ya Jumamosi Agosti 01 kumkabidhi tawasifu yake. "Kwenye mkutano huo licha ya kuumwa kwake, Papa alikuwa na matumaini na kusema kwamba endapo hali yake itaimarika, atachukua kalamu tena aandike," limeandika gazeti hilo. Papa Benedict alimtembelea kaka yake aliyekuwa mgonjwa aitwaye Georg nchini Ujerumani mwezi Juni,ikiwa ziara yake ya kwanza nje ya Italia tangu alipojiuzulu ghafla upapa mwaka 2013. Georg Ratzinger alifariki dunia wiki mbili tu baada ya hapo akiwa na umri wa miaka 96. Papa huyo wa zamani, ambaye jina lake halisi ni Joseph Ratzinger,sasa anaishi kwenye nyumba ndogo ya watawa mjini Vatican. Tangu awe Papa wa kwanza kujiuzulu kwa takribani miaka 600 iliyopita,amekuwa haonekani sana hadharani kutokana na hali yake ya kiafya. Akiwa mwanamapokea ya kanisa katoliki, nafasi yake ilichukuliwa na mwanamgeuzi Papa Francis.
More Episodes
Mziki mzuri na maelezo ya wasani mbalimbali yana patikana hapahapa jamsingi subscribe ili uwe wa kwanza kupata vibes connection
Published 11/16/20
Published 11/16/20
"COUNTRY BOY" AZUNGUMZIA UMUHIMU WA MSANII KUWA TRENDING YOUTUBE NA VIEWS WENGI KWENYE MUZIKI WAKE.
Published 11/10/20