WATU ZAIDI YA MILIONI 1.8 WANATAFUTA HIFADHI NCHINI UJERUMANI.
Description
Idadi ya watu wanaotafuta hifadhi nchini Ujerumani kutokutoka na vita ama mateso katika nchi zao iliongezeka kupita milioni 1.8 mwishoni mwa mwaka jana kulingana na takwimu rasmi zilizotolewa tarehe 23, Julai.
Idara ya takwimu ya serikali kuu (Destatis) imesema kuwa nb idadi hiyo iliongezeka kwa kiwango cha chini cha kila mwaka kutoka asilimia 3 mnamo mwaka 2012, idadi hiyo ilijumuisha raia wa kigeni ambao walikuja nchini Ujerumani kwasababu za kisheria, kisiasa ama kibinadamu.
Mnamo Desemba 31, takribani watu 266000 miongoni mwa waomba hifadhi hao walikuwa bado wanasubiri uamuzi wa mwisho wa maombi yao ya kutafuta hifadhi, idara hiyo ya (Destatis) imeripoti kuwa kiwango hicho ni asilimia 13 chini ya kile kilichoshuhudiwa wakati sawa na huo wa mwaka jana.
Hii inahusishwa na ufanisi uliopatikana katika kazi iliyoko pamoja na kupunguzwa kwa ujumla wa kiwango cha maombi ya kutafuta hifadhi.