MAMBO MATATU AMBAYO NI SUMU KATIKA MAHUSIANO YA KIMAPENZI.
Description
Katika harakati zako za kutafuta mpenzi, unaweza kukutana na mwanamke ambaye kwasababu moja ama nyingine anakuondolea uwezo wako wa kufikiri, kutumia mantiki na pia kutumia akili yako ya kuzaliwa.si lazima awe amekufanyia kitu, lakini inaweza kuwa ni ulevi wako tu unasababisha ufanye mambo yasiyo ya kawaida.pengine ndio maana baadhi ya wasanii huzungumzia suala la "kudata" kutokana na mapenzi.
Ni jambo jema kudhani kuwa wewe na mpenzi wako mnapendana kwa dhati na kwamba kila mmoja amefika kwa mwenzake, lakini kama moja wapo ya mambo haya yaliyoelezwa hapa chini litajitokeza basi fahamu kuwa yamkini unependa kuliko kawaida, yaani ni kama umenyweshwa sumu ya penzi.kumbuka kupenda ni kuzuri, lakini kupenda kupindukia kunaweza kukutumbukia nyongo kwani katika kila jambo kunahitajika kiasi.
Yafuatayo ndio mambo ambayo ni sumu katika mahusiano ya kimapenzi
Kumuingilia mpenzi wako katika mambo yake
Unaweza kujikuta ukisumwa kumwambia mpenzi wako awe anavaa nini kwa wakati gani, akutane na nani kwa wakati gani au ale nini.ukiona fahamu kuwa hayo si mapenzi, bali umepitiliza na pengine mwisho wa uhusiano wenu unanukia.
Hata ukiachilia mbali suala zima la usawa wa kijinsia, hakuna mwanamke angependa apangiwe kila kitu kuhusiana na maisha yake, kama ilivyo dokezwa hapo juu kila mtu ana maisha yake na kilichowaunganisha ni mapenzi tu.kama unataka kumpangia kila kitu ni wazi utaishia kuishi pekee yako.
Kutompa nafasi mpenzi wako
Kama huishi na mpenzi wako ni jambo la kawaida kuwa na hamu ya kumuona mara kwa mara, lakini kumbuka kuwa mpenzi wako naye ana maisha yake na anahitaji nafasi ya kuwa pekee yake kwaajili ya mambo yake binafsi.
Hisia za kutaka kuwa na mpenzi wako muda wote zinaweza kudhaniwa kuwa ni za mapenzi ya dhati, ila kwa hakika hiyo siyo ishara njema ya mapenzi ya kudumu. hebu jiulize kama unaweza kuendeleza hali hiyo maisha yako yote.
Ni wazi kuwa utachoka, kwahiyo mpe mpenzi wako fursa ya kupumua.namna hii mpenzi wako atajenga hamu ya kukutana nawe lakini ukiwa naye muda wote hamu itaisha.
Wivu kupindukia
Ni jambo jema kwa mwanamume kumtakia heri mpenzi wake na kufanya kila awezalo kuhakikisha kuwa hapati madhara, lakini iwapo utakuwa mtu wa wasiwasi na mashaka pale unapomuona mpenzi wako akizungumza na mwanaume mwingine,au anapotoka na marafiki zake wa kike,au anapovaa nguo inayomfanya atamanishe, basi fahamu kuwa unakunywa sumu ya mapenzi.
Katika uhusiano wa kimapenzi, kuaminiana ni jambo muhimu sana.kama kweli unataka Mpenzi yako akupende kwa dhati,mwonyeshe kuwa unamwamini na unaheshimu maamuzi yake ikiwa ni pamoja na maamuzi ya kutoka na marafiki zake wa kike na kuwa na marafiki wa kawaida wa kiume. Ondoa hofu na acha kabisa kumpeleleza, maana wapo wanaume ambao hutumia muda mwingi kuwapeleleza wapenzi wao ikiwa ni pamoja na kuwategeshea kamera na rekoda za simu.
Kama ukizingatia mambo haya machache katika mahusiano yako ya kimapenzi na kama kweli mnapendana na mnamalengo ya kufika mbali na mahusiano yenu basi zingatia haya na utayafurahia mahusiano yenu na yatakuwa mfano wa kuigwa na watu wengine.