HUAWEI YAPIGWA MARUFUKU KUWEKA MITAMBO YA 5G NCHINI UINGEREZA.
Description
Uingereza imepiga marufuku Kampuni ya Huawei kuweka mitambo ya 5G huku kampuni kama BT (BTGOF) na Vodafone (VOD) zikipewa muda mpaka 2027 kuondoa mitambo ya kampuni hiyo kwenye mitandao yao.
Waziri wa masuala ya kidigitali na Utamaduni, Oliver Dowden amesema kutokana na hali ya sintofahamu inayozunguka Kampuni hiyo ya china, Uingereza imekosa imani na mitambo ya 5G ya Huawei.
Marufuku iliyotolewa na Uingereza ni ushindi mkubwa kwa Marekani ambayo imekua ikishinikiza Mataifa kupiga marufuku Kampuni hiyo kwa madai kuwa ni tishio kwa usalama wa taifa.
Uamuzi wa Uingereza umetejwa kuwa ni pigo kubwa sana kwa kampuni ya Huawei kwani soko muhimu kwa kampuni hiyo na 24% ya mauzo ya mwaka jana yalitokea huko.
Vilevile Kampuni hiyo ya kichina ambayo imeanza kuzalisha bidhaa za mawasiliano tangu mwaka 1997 bado inaendelea kufanya vizuri sokoni kwa kuleta bidhaa mpya za simu na tablets.