CHINA : NYAMA YA KUKU YAKUTWA NA VIRUSI VYA CORONA.
Description
Sampuli ya vipapatio / mabawa ya kuku yaliyogandishwa, zimegundulika kuwa na virusi vya Corona mjini Shenzhen. Nyama hizo ziliagizwa kutoka nchini Brazil.
Baada ya ugunduzi huo, mamlaka za afya ziliwatafuta na kuwapima watu waliokuwa karibu na bidhaa hiyo ambapo majibu yamesema kuwa hawana maambukizi.
Aidha eneo ambalo vipande vyenye virusi viliwekwa limepuliziwa dawa na mamlaka inatafuta bidhaa zingine za kampuni hiyo ambayo bado haijawekwa wazi.
Hata hivyo shirika la Afya Duniani (WHO) na kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa Marekani (CDC) zimewahi kusema uwezekano wa kupata Corona ni mdogo kupitia chakula.
Taarifa hiyo ya kupatikana kwa Covid-19 kwenye mabawa ya kuku, imekuja huku siku moja tu nyuma yake nchini Ecuador kulipatiana virusi vya Corona kwenye samaki wadogo wa baharini aina ya uduvi wakiwa kwenye moja kati ya migahawa nchini humo kwaajili ya kuuzwa kwa wateja.
Mpaka sasa taifa la China limeripoti kuwa na visa 84,786, huku Brazil ikiwa na nchi ya pili kuwa na maambukizi makubwa ya Covid-19, kwa kuwa na visa Milioni 3.1 na taifa la Marekani likiwa linaongoza kwa kuwa na visa Milioni 5.26