NEW ZEALAND : ALIYEUA WAUMINI 51 MSIKITINI AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA.
Description
Mahakama imemhukumu kifungo cha maisha jela bila uwezekano wa msamaha Brenton Tarrant(29) aliyeua watu 51 kwenye misikiti miwili nchini humo.mtoto mwenye umri wa miaka 3 alikuwa miongoni mwa waliouawa.
Machi mwaka jana, waumini waliokuwa wanasali katika msikiti wa Al Noor na Linwood walishambuliwa na Tarrant ambae alirusha tukio hilo mubashara Kupitia mtandao wa facebook.
New Zealand haina adhabu ya kifo na Jaji Cameron Mander amesema hukumu hiyo hutolewa kwa wauaji wabaya zaidi,akiongezea kuwa kitendo kilichofanywa na mtuhumiwa hakikuwa na ubinadamu.
Hii ni kwa mara ya kwanza kwa hukumu ya aina hiyo kutokewa katika historia ya New Zealand.Mtuhumiwa ambae ni raia wa Australia alikiri kufanya mauaji hayo na kujaribu kuuwa wengine 40.