TABIA ZA WATU WENYE USALITI KATIKA MAHUSIANO YA KIMAPENZI.
Description
Usaliti ni jambo baya sana katika mahusiano, usaliti si ujanja japo wengi wanaowaza kusaliti huwa wanajiona wajanja.wanajiona wamefanikiwa pale ambapo wanasaliti wenza wao kutogundua kama wanasalitiwa.
Siku zote anaekusaliti huwa anajiona mjanja sana, kwamba yeye anasaliti mwenza wake hasaliti. Kwa asilimia kubwa wanaume hujiona kama usaliti ni halali yao, wanataka wao wasaliti lakini wapenzi nb wao wasithubutu kuwasaliti.
Kwanini hawataki wenza wao wasaliti? eti wanaumia, hakuna kitu kinacho mchukiza mwanaume kama kusalitiwa.
kusaliti asaliti yeye akisaliti mwenzake ni kosa la jinai anaona amedhalilishwa
Anajisikia fedheha kwamba Mpenzi wake amemuonaje? amemchukuliaje?hajakamilika idara gani? Anawaza sana na kujiuliza jamii nzima inayojua kitendo hicho inamtazamaje?.
Hapo ndio unakuta mwanaume anaamua kuchukua uamuzi mgumu ikiwemo hata kuhatarisha maisha ya mwenza wake.
Zifuatazo ni dalili za usaliti.
1. KUTOPENDA KUFATILIWA KIUNDANI.
Mara nyingi anaekusaliti hapendi kuchimbwa mambo kwa undani, anahofu anaweza kuchanganya madawa, hapendi mazungumzo mafupi ya moja kwa moja.
Hapendi kuulizwa maswali mengi, ukimuuliza anayakwepa na kutaka kukupeleka kwenye mazungumzo anayoyataka yeye.
Ukimuuliza Kuhusu mipango yenu, ukimuuliza Kuhusu mustakabali wa mahusiano yenu hawezi kukujibu moja kwa moja baada huku ondoa kwenye mstari na kukufanya usiwe na hamu ya kumuuliza.
2. HAPENDI UJUE RATIBA ZAKE.
Mara nyingi mtu ambaye ana mambo yake hapendi ujue ratiba zake, anataka usimzoee ,iwe anafanya maamuzi yake kulingana na yeye mwenyewe anavyotaka, ikitokea unaijua ratiba yake atakuwa ni mtu wa kutoa udhuru kila wakati.
Leo atakwambia kuna mgonjwa anakwenda kumuona, kesho atakwambia kuna kikao cha wafanyakazi wenzake, siku nyingine atakwambia gari imepata pancha analazimika kusubiri mafundi hadi wafike ndio aweze kuanza safari.
3. SIMU YAKE NI KITUO CHA POLISI.
Anayesaliti mara nyingi hapendi kuacha simu yake kiholela, simu inakaa mfuko kwake hata kama hakuna ulazima wa kufanya hivyo mpo nyumbani kwenye kikao cha mazungumzo ya kifamilia yeye simu yake ipo mfukoni.
Imetolewa mlio hataki usikie ikiita, au ujumbe ukiingia ,au picha na mambo mengine ya kimapenzi.
Anayejiamini na yupo kwenye uhusiano imara hana sababu ya kuficha ficha simu yake au kuweka paswedi kila mahali simu yake anaiweka hadharani.
Mwingine anakusetia simu yake ukimpigia kila wakati inaonekana inatumika wakati huo anakusaliti.
4. ANACHATI SANA.
Wanaosaliti wengi wao hupenda kutumia meseji katika mawasiliano yao, yaani anawazoesha michepuko yake wote kusaliti hapendi kupokea simu zaidi anapenda kuchati hivyo ni rahisi kuchati na wapenzi wengine bila wewe kujua na kufuta meseji zote ili hata ukishika simu kwa bahati mbaya usizione na usigundue kitu.
Mwisho hakutambulishi kwa watu wake wa karibu, ukiona mpenzi wako hajawahi kukutambulisha kwa rafiki zake, ndugu zake na watu wengine wa karibu ujue hapo hamna muelekeo wa mapenzi yenu tafuta njia mapema ya kujiundoa kabla ya kupotezewa muda wako.
Kwa haya machache natumaini utakuwa umeshafahamu Mpenzi wako uliyenae kwa sasa ana malengo gani? na je anakusaliti ama ni mwaminifu ili uweze kuchukua hatua mapema kabla mambo hayajaharibika.