SE7EP38 - SALAMA NA MFAUMEX2 | TOE - TO - TOE
Listen now
Description
Mfaume Mfaume ni yule mwana ambaye akitokea sehemu ni sahihi kwako kuwaambia wahusika kwamba jamani, mwamba huyu hapa! Muonekano wake pekee unamfanya mtu ajue yuko kwenye presence na mtu maalum na baadae ukishajua hasa nini anafanya basi huwezi ku doubt yote ambayo utaambiwa juu yake lakini kubwa zaidi ukipata sasa nafasi ya kumuona anapokua kazini kwake hapo ndo utakaposhia kumpa nyota zake zote anazostahili kama bondia. Tena popote pale, iwe akiwa gym au ulingoni ambapo kadhaa washachezea shurba kutoka kwake. Mfaume ni kama wengi wetu ambao tumetokea katika familia za kawaida tu ambayo malengo ya wazazi wetu kwetu ni kuhakikisha unasoma ili uweze kupata kazi nzuri na uje uwasaidie wao na Ndugu zako utakapokua mkubwa, vile vile mambo ya michezo ni kawaida maana kama mtoto unapokua unakua shuleni na mtaani ni lazima kunakua na kucheza, chochote ambacho kiko mbele lakini zaidi huwa ni mpira wa miguu kwa Kaka zetu ingawa sasa dunia imebadilika kiasi, siku hizi hata watoto wa kike kucheza soka ni jambo la kawaida tu na kwa hilo napenda sana. So kwa Mfaume ni kama kwetu wengine tu, alianza kwa kucheza mpira lakini baadae interest yake ikatoka kutoka kwenye mpira na kuhamia kwenye ngumi, kwa wazazi wake huo ulikua mitihani hasa. Kwa mzazi kukuona mtoto wake akichezea vitasa mara kwa mara haliwezi kuwa jambo la kupokelewa kwa mikono miwili ndani ya nyumba, mtoto anarudi nyumbani kutoka kujifua nae anakua kafuliwa kwelikweli au akijua kwamba una pambano na mwamba flani aliye shindikana ndo hofu inapanda mpaka juu ya dari na inaeleweka kwanini inakua hivyo na kama mpaka sasa hujaelewa au hujaipatia picha basi mwenzetu huna moyo lol. Alinipa story moja kwenye maogezi yetu haya kuhusu Mama yake, ananiambia kuna wakati alikua na mechi na bondia ambaye alikua anaongea sana, anajisifia na kumtishia sana maisha yake, kwamba atamchakaza vibaya sana tena mbele ya Mama yake, na aliyasema hayo akijua fika Mfaume huwa anaenda na Bi Mkubwa wake kwenye fight zake zote za ndani, ananiambia Mama yake aliogopa sana, alimsihi sana lakini kwa jitihada zake na maguvu ya Allah aliweza kumaliza mchezo wake huo vizuri tu. Mabondia ni watu ambao wana roho za kipekee sana, unaweza ukamkuta mtu akiwa uliongoni anatoa dozi nzito kwa mpinzani wake ukadhani ni mtu mwenye roho mbaya sana, lakini ukimkuta nje ya ulingo na kwa watu wake utajua ni mtu wa aina nyengine kabisa. Kwa bahati nzuri nna marafiki ambao wanacheza mchezo huu wa boxing ikiwa pamoja na Mfaume mwenyewe, huwa ni watu wakarimu sana na wana mapenzi ya kweli lakini akiwa uliongoni anakua mtu mwengine kabisa, nadhani hiyo ndo tofauti ya masumbwi na michezo mengine. Yangu matumaini uta enjoy session yetu hii ya mwisho ya msimu huu na mwana huyo humble kutoka kitaa, na pia kama kawaida utaokota mawili matatu ambayo yatakusogeza sehemu. Tafadhali enjoy. Love, Salama. --- Support this podcast: https://podcasters.spotify.com/pod/show/yahstonetown/support
More Episodes
Published 03/02/23
Toufiq ni moja ya majina makubwa kati ya wafanya biashara wazuri na sasa mwanasiasa na Mbunge wa Mpendae, kwa wazee na vijana wa visiwani humo yeye ni mmoja wa mifano ya kuigwa ingawa kwake yeye yaliyo mengi kwenye maisha yake ni nguvu kubwa ilifanywa na Marehemu Mzee wake Ndugu Salih Hassan...
Published 02/23/23
Kwenye jiji la ‘Maraha’ hapa nyumbani kwetu Tanzania ambayo kwa miaka ya hivi karibuni sehemu za starehe zimekua tele na kila mmoja ana uwezo wa kula bata zake vizuri tu kulingana na urefu wa mfuko wake basi hakuna ambaye HAJUI jina la DJ huyu mahiri ambaye kwa ubunifu wake ameweza sana...
Published 02/16/23