Episodes
Mfaume Mfaume ni yule mwana ambaye akitokea sehemu ni sahihi kwako kuwaambia wahusika kwamba jamani, mwamba huyu hapa! Muonekano wake pekee unamfanya mtu ajue yuko kwenye presence na mtu maalum na baadae ukishajua hasa nini anafanya basi huwezi ku doubt yote ambayo utaambiwa juu yake lakini kubwa zaidi ukipata sasa nafasi ya kumuona anapokua kazini kwake hapo ndo utakaposhia kumpa nyota zake zote anazostahili kama bondia. Tena popote pale, iwe akiwa gym au ulingoni ambapo kadhaa washachezea...
Published 03/02/23
Published 03/02/23
Toufiq ni moja ya majina makubwa kati ya wafanya biashara wazuri na sasa mwanasiasa na Mbunge wa Mpendae, kwa wazee na vijana wa visiwani humo yeye ni mmoja wa mifano ya kuigwa ingawa kwake yeye yaliyo mengi kwenye maisha yake ni nguvu kubwa ilifanywa na Marehemu Mzee wake Ndugu Salih Hassan Abdullah Turky aka Mr White ambaye na yeye akiacha ukweli kwamba alikua tajiri na mfanya biashara nzuri huko visiwani ila yeye pia alikua kipenzi cha wananchi wa Jimbo la Mpendae ambapo sasa Toufiq ndo...
Published 02/23/23
Kwenye jiji la ‘Maraha’ hapa nyumbani kwetu Tanzania ambayo kwa miaka ya hivi karibuni sehemu za starehe zimekua tele na kila mmoja ana uwezo wa kula bata zake vizuri tu kulingana na urefu wa mfuko wake basi hakuna ambaye HAJUI jina la DJ huyu mahiri ambaye kwa ubunifu wake ameweza sana kubadilisha kabisa jinsi ambavyo wenzake walomtangulia walikua wanafanya. Yaani Ally alikichukua kitabu cha jinsi ya kutoa burudani kama DJ na kukichanachana na kisha akaanza kuandika cha kwake, ambacho mpaka...
Published 02/16/23
Ulikua muda mwingi hasa umepita toka mara ya mwisho nilionana na Evans wa Bukuku na kukaa naye chini kisha tukaongea. Na ki ukweli hajawahi kuwa rafiki yangu wa karibu ila ni mtu ambaye tunafahamina na kuheshimiana. Hustle zake nazifahamu kwa ukaribu maana industry ambayo tunafanya kazi ndo hiyo hiyo kwahiyo nikama chakula, tusipokutana jikoni basi tutakutana kwenye sahani. Kama ilivyo kwa watu wengi nimekua nikimsikia kwenye radio mbali mbali katika safari yake kama mtangazaji wa vipindi...
Published 02/09/23
Kwa ambao wanafuatilia mpira hapa nyumbani wanamjua mchezaji huyu mahiri wa Simba Queens lakini ambao wanafuatilla soka la wanawake hawa watakua wanaelewa uwezo binafsi na uhodari wake wa kucheza namba tofauti tofauti uwanjani ila ukimkuta kaikamata mbavu ya kulia aidha kwa Simba au timu ya Taifa ya Tanzania. Fatuma Issa ni mtu na nusu, hakuna mpenzi wa mpira au kocha yoyote wa mpira anaweza akamuacha kwenye benchi wakati team inatafuta matokeo au inataka kuwaonyesha walofika kuwaangalia...
Published 02/02/23
Kheri Sameer aka Mr Blue aka Lil Sama aka Bayser ni mdogo wangu, mdogo wangu kabisa na uzuri nakumbuka kabisa mara ya kwanza kuonana nae na mpaka alivyokua amevaa. Jezi ya Denver Nuggets, jeans ya light blue na sneakers nyeupeeehh na chain ya Silver, kwenye maskio alikua na hereni za kung’ara zile ambazo zilikua si za kitoboa skio, zilikua zina smaku na nazijua zaidi kwasababu Marehemu cousin brother wangu alikua nazo maana nyumbani ilikua hairuhusiwi kutoboa maskio enzi hizo. Alikua msafi,...
Published 01/26/23
Mrisho Halfani Ngassa alikua top top top footballer na kwa bahati nzuri nishawahi kumshuhudia akiwa kazini kwake, tena ukimkuta kaamka vizuri basi uhakika wa burudani ni UHAKIKA . Na kipindi ambacho alikua kwenye peak yake pia kulikua na vitasa imara na magolkipa wazuri tu lakini nna uhakika kila mmoja kati yao ana la kusema kuhusu winga na forward hii machachari ambayo nchi yetu ishawahi kuona. Hakuna kitasa ambacho hakijawahi kukataa kufungua mlango muda ambao Mrisho Ngassa alikua anakuja...
Published 01/19/23
Kutoka zake Lushoto huku mkoani Tanga ni kijana mtanashati ambaye anajua kama amekuja town au jijini Dar es Salaam kwasababu ya kusaka pesa ili abadilishe maisha yake na ya wale ambao wamemzunguka. Na kila alikumbuka ambapo ametoka basi spidi ya kuhakikisha kalamu yake haivuji na inaandika kwa muandiko mzuri ili kila ambaye atabahatika kusoma kile ambacho yeye kakiwaza na kukiandika basi azame kwenye dimbwi lake na endelee kumsikiliza mpaka pale yeye mambo yake yatakapoenda, na kwa story...
Published 01/12/23
Ushawahi kumuangalia mtu kwa mbali na kujiuliza maswali mengi juu yake? Maswali kama siku yake ikoje, amewezaje? Kama ana familia? Ki kawaida huwa anaamka saa ngapi? Amesoma wapi? Siku yake anaipangaje? Ana watoto? Mtoto? Huwa anawaandaa kwenda shule? Muda je wa kukaa nao? Elimu yake ameipatia wapi? Kwenye familia aliyotoka je? Wazazi wake wapo? Na je wanajivunia yeye kwa kiasi gani? Sasa ili kupata majibu ya maswali hayo yote ilibidi tumtafute Bi Brenda Msangi-Kinemo ambaye ndo nilikua...
Published 01/05/23
 Deo Gratias, jina tu linatosha kujielezea kama wewe nawe utakua kama mimi wa kutaka kujua maana ya majina ya watu ili uweze kujua tabia zao au ujiulize wazee wake walikua wanafikiria nini wakati wanaamua kumpa jina hilo mtoto wao. Kwa Deo maana imejibeba na imejikamilisha na kwa yeye kuamua kubaki na jina lake hilo hilo mpaka kwenye stage ambako ndo sehemu yake ya kazi inabidi hilo nalo likuambie jambo kuhusu yeye na jinsi ambavyo anajichukulia na kuyachukulia mambo ambayo ameyachagua...
Published 12/29/22
Jina MC Gara B ni miungoni mwa majina makubwa sana kwenye ulimwengu wa kazi ambayo mwenzetu huyu amechagua kuifanya. Familia yake, mke na watoto, wazazi wake na wa mkewe pengine, Ndugu jamaa na marafiki na waajiriwa wake wanakula vizuri kwasababu ya kipaji chake Ndugu yetu huyu. Ni mwanaume ambaye akiwa kazini kwake furaha na burudani ambayo huwapa wateja wake ndo inayomfanya azidi kuenda mbali kwenye tasnia hiyo ya ushereheshaji. Again, yeye ni mmoja ya BORA kadhaa ambao wanafanya kazi kama...
Published 12/22/22
Baraka Kizuguto si moja ya majina yajulikanayo miungoni mwa wa Tanzania wengi ambao asilimia kubwa ya wenye simu za mkononi hupendelea zaidi habari za maisha ya watu maarufu na mashuhuri, kutaka kujua wanakula nini, wanaishi wapi, wanalala wapi, wanalala na nani na kadhalika. Na kama wewe ni mmoja wa watu hao na si mpenzi wa mpira basi kumfahamu mgeni wetu wa kwenye kiti chakavu wiki hii itakuwia vigumu. Ila kwa wale watu wa mpira, au wafanyakazi kwenye Vyama vya mpira hapa kwetu na Afrika...
Published 12/15/22
Habibi Masoud Kipanya ni Ally Masoud Nyomwa ambaye ni LEGEND. Kwa mujibu wake alizaliwa huku kakunja ngumi na dhana yake ni kwamba alizaliwa ili awe bondia! Kwa anacho kifanya na ambacho amekua akikifanya tena kwa ufasaha kwa miaka nenda miaka rudi bila ya shaka ni UBONDIA. Hakuna ambaye atabisha juu ya hilo. Amekua akipigania mambo tele na kuyasemea mengi pamoja na kuchekesha na kuelimisha kupitia kalamu yake. Kwa mujibu wake yeye ni mbobevu katika taaluma ya kupuuza na kuchukulia mambo poa...
Published 12/08/22
Kuna mambo mengi wakati mwengine ambayo yanakua yanaendelea au yalitokea kwenye maisha ya baadhi ya watu ambao huja kukaa kwenye kiti chetu chakavu na meza yenye kigae. Ila kwasababu zilizo wazi za kuwataka wasijisikie uncomfortable na pengine kuwafanya hata ambao wangependa au ambao tungependa waje nao wasijiskie hivyo ndo kanuni ambayo tumeamua au niseme niliamua kipindi huko nyuma kuifuata. Nia na madhumuni ya session zetu hizi zaidi ni kuwapa watu maua yao wakiwa hai, sisi nasi kuskiliza...
Published 11/30/22
Doris Mollel kwa kuanzia tu tuanze na jina lake, ni zuri lenye kukumbukwa ki rahisi, yeye mwenyewe pia ni mrembo na mkarimu, sana. Roho yake ni kama rangi yake, nyeupe na kwa bahati Mimi namfahamu yeye kiasi kwa kupitia rafiki zangu ambao yeye anafanya nao kazi na pia ana mahusiano nao mazuri, sana. Pia namfahamu mume wake ambaye tukianza shindano la kumtafuta nani mkarimu kati yao tunaweza kukamaliza kwa suluhu. Huwa naamini Mwenyezi aliwakutanisha ili kwa pamoja waweze kufanya makubwa...
Published 11/24/22
Pengine jina la episode hii linaweza likakupa muangaza kidogo wa story fupi ya maisha ya mgeni wetu wa wiki hii kwenye kiti chetu chakavu na meza ya kigae ambaye leo hii tayari kashaona, tochi ya maisha kwake inamulika tu vizuri na mbele anapaona. Huyu ni Walter Chilambo ambaye miaka tuseme 14 iliyopita alikua hana uhakika wa chakula chake cha siku tu achana na sehemu gani atalala. Ruka ruka ya kule na huku na bahati ya kupendwa alonayo na ambayo inaendelea mpaka leo naamini inakuja kwasababu...
Published 11/17/22
Nilipoandikiwa ujumbe mfupi na Edwin Bruno ambaye ni mkwe wa Professor kwamba Mama amekubalia kufanya kipindi na sisi siku hiyo ya Jumapili akishatoka church nilihisi kama naota. Mwenyezi Mungu anajua kwa kiasi gani tumekua tukitaka kufanya maongezi nae kwenye kipindi chetu. U busy wake na pengine mara nyingi kutokuwepo Dar es Salaam napo palikua panaleta ugumu, nyengine ilkua ni tarehe zetu za kufanya production na availability yake zilikua zinapishana sana. So unaweza ukaelewa excitement...
Published 11/10/22
Katika pita pita zangu siku si nyingi nilimsikia mtu akimzungumzia mgeni watu wa wiki hii kwamba ni ‘Jay Z’ wa Bongo na si kwasababu kamuoa mmoja wa wasanii hodari wa kike na ambao wako juu ki muziki, ila pia akili yake ya kibiashara kwa kiasi kikubwa imemfanya yeye aone hivyo. Kwa ufahamu wangu niliambiwa na kushuhudia suala la maneno na mawazo ‘kuumba’. Pale mtu au watu wanapo kuona na ukichanganya na juhudi zako na nia na madhumuni ya wewe kutaka kufika pale basi mengine kutimia huwa ni...
Published 11/03/22
Ushawahi kuwa na mtu ambaye mnafahamiana vizuri miaka nenda na miaka rudi na hata pengine kwa u busy wa maisha zikapita siku hamjaongea lakini unajua yuko sawa yeye na Familia yake na mambo yanaenda vizuri, na kama isingekua hivyo basi ungekua ushajua? Ambaye unajua kukiwa na situation flani basi yeye anatafanya jambo flani na kuzima au kuwasha moto, na kama kuna neno umeambiwa kasema unajua kabisa ni kweli au si kweli? Au kama una suala unataka kulifahamu vizuri linalohusu mambo fulani na...
Published 10/27/22
Lameck Ditto Sr ni Baba, Mwalimu, mwanamuziki, muandishi, mentor, mume na zaidi ya yote ni mwana tu ambaye maisha alopitoa kipindi anakua hayajawahi na wala hayatawahi kumsahaulisha yeye ni nani na wapi ambapo ametokea na wapi anataka sana kuelekea maana huko ndo kwenye kesho yake, na kwa kumsikiliza ambavyo nimemsikiliza, kesho yake anaithamini sana na amekua akiiandaa vizuri ili hata siku moja asije akakwama na kuanza kuishi maisha ya jana ambayo yalikua si mazuri hata kidogo. Yeye na Baba...
Published 10/20/22
Hii nayo ni moja ya zile ambazo ziliuliziwa sana na kwa muda mrefu nasi kwa upande wetu tumekua tukiifukuzia tuweze kukaa na mwamba huyu hodari kutoka Zanzibar. Mimi mwenyewe ambaye nimekua nikifanya kazi kwenye kiwanda hiki cha burudani nilikua na hamu ya siku moja kuwa kwenye meza moja na Ndugu yangu huyu, kuweza kumtazama usoni na kumuuliza yote ambayo nilikua nataka kumuuliza kwa kipindi kirefu sana. Maana hata mimi nimekua nikimsikiliza miaka nenda miaka rudi na siku zote emeemdelea...
Published 10/13/22
Katika binadamu ambao walinipa wakati mgumu na kusubiri kwingi kabla ya kuja kukaa kwenye meza yetu ya kigae na kiti chakavu basi mmoja wao ni Rose huyu wa Muhando. Upatikanaji wake ni kama ukitaka kumuona SIMBA mbugani, lazima uamke asubuhi na mapema au uwe na bahati ya mtende kama ambayo sisi tumepata. Ingawa tulisubiri kwa masiku tele na miezi tele katikati ya mwaka huu tuliweza kumpata na kukaa nae chini ili tuweze kuzungumza nae. Rose ni wa moto sana, kalenda yake imejaa safari tele za...
Published 10/06/22
Zahir Ally Zorro ni mkongwe wa muziki wa dansi na kwa habari ambazo nimepata ni kwamba enzi zake alikua wa moooto sana tena kwenye kila nyanja, kuimba, kuandika, kupiga gitaa na mpaka uvaaji, alikua handsome boy sana na ulimbo kwa kina Dada enzi hizo. Utashi na ucheshi na u sharp wake ndo ambao ulikua unamfanya asimame PEKEE kwenye kadamnasi ya wanamuziki wengi wa kipindi hiko. Naomba nikukumbushe pia kwamba enzi hizo zilikua pia si za kuzichukulia poa kabisa, maana ushindani wa bendi na...
Published 09/30/22
Kipindi cha nyuma kidogo nilifanya lile ambalo huwa nafanya la kuwashirikisha rafiki zangu na team kuhusu list ya watu ambao wangependa kuwaona kwenye kiti chetu chakavu na sababu za kwanini hasa waje kwenye meza ile yenye kigae kwa juu maana tukisema tutaje majina tu bila ya sababu thabit za wao kuja pale tunaweza tukaondoa maana yenyewe ya kuwa na watu wenye story za kuvutia na kutufunza kama ambavyo tumekua tukifanya. Jina la mgeni wetu huyu lililetwa kwangu na Michael (Mx) Mlingwa na...
Published 09/22/22