SE7EP26 - SALAMA NA MASOUD KIPANYA | HERI KUFA MACHO…
Listen now
Description
Habibi Masoud Kipanya ni Ally Masoud Nyomwa ambaye ni LEGEND. Kwa mujibu wake alizaliwa huku kakunja ngumi na dhana yake ni kwamba alizaliwa ili awe bondia! Kwa anacho kifanya na ambacho amekua akikifanya tena kwa ufasaha kwa miaka nenda miaka rudi bila ya shaka ni UBONDIA. Hakuna ambaye atabisha juu ya hilo. Amekua akipigania mambo tele na kuyasemea mengi pamoja na kuchekesha na kuelimisha kupitia kalamu yake. Kwa mujibu wake yeye ni mbobevu katika taaluma ya kupuuza na kuchukulia mambo poa kwa kipindi sasa. Lakini pia anaamini yeye ni MTATA. Tukienda mbele na kurudi nyuma, hapo kwenye UTATA hakuna ambaye anaweza kumbishia, hasa kwa wale ambao kalamu yake imewanyoosha kwa kiasi kikubwa. Mimi na yeye tulikutana kwa mara ya kwanza takriban miaka kumi na tisa iliyopita, wakati huo mimi mbichi hasa na yeye akiwa kashajielewa na chemchem yake ya kipato tayari ilikua inatoa neema. Mimi nilikua ndo kwanza naanza kazi ya kujishikiza pale Times FM kipindi hiko bado ilikua kule Kamata. Masoud alikua analichorea gazeti la Majira ambalo lilikua liko kwenye mwamvuli mmoja na Radio ambayo nami nilikua nimejishikiza baada tu ya kumaliza skuli. Urafiki wetu ulikuja naturally tu maana sote tunapenda kucheka. Kupitia Zuhura Yunus na Binti mwengine wa kuitwa Rahma ndo mimi naye tulifahamiana. Wakati huo yeye alikua na gari kwahiyo lifti za hapa na pale zilikua hazikauki. Pia tulikua tunaitumia gari yake kama sehemu ya ku chill na kuskiliza muziki kwenye parking za Times FM. Huwezi kukaa kwenye tasnia moja kwa muda mrefu kama wewe si hodari na mwenye kujielewa. Moja ya vitu ambavyo naviusudu kutoka kwake ni uelewa wake wa mambo tele wa tele, IQ yake ni ya juu sana na jinsi ambavyo ana reason ndo huwa anamaliza kabisa, kama binadamu wakati mwengine ni bora kukubaliana kuto kukubaliana na kwakwe yeye wakati mwengine jinsi anavyo wachora baadhi ya matukio na watu huwa haviishii kuzuri lakini hiyo haikuwahi kuwa sababu ya yeye kuacha kufanya ambacho anakifanya na ambacho amekua akikifanya kwa muda sasa. Uelewa wake kwenye mambo ambayo yanaendelea, uwezo wake wa kuona mbali na kuweka sanaa yake hiyo kwenye karatasi kisha kutuachia sisi tung’amue maana yake kwa kweli ni kipaji cha kipekee ya sana. Mmoja anatakiwa akae tu mbali na ku admire akifanyacho na hiko ndo ambacho mimi nimeamua kufanya. Nilikua nataka anielezee maana halisi ya baadhi ya michoro yake ambayo iliacha gumzo kwa muda mrefu lakini kwa sababu ambazo niliziheshimu alisema asingependa iwe hivyo, uhuru wa kuwaacha watu watafsiri wao ndo raha ya kazi yake ingawa yeye anajua hasa kwanini alichora na maana yake hasa ni nini! Kwa heshima ya sanaa ilibidi nikubali matokeo. Toka umeanza kumjua na kufuatilia kazi yake, mara ngapi ushawahi kuskia Masoud yuko matatani? Yaani kakamatwa au hajulikani alipo? Kwangu mara kadhaa lakini haikuwahi kuwa kizuizi cha yeye kuacha kufanya afanyacho, kuogopa je? Nadhani kama binadamu kuwa na uoga ni jambo la kawaida, ila unafanyaje baada ya hapo ndo tofauti yetu. Episode hii inajumuisha karibu yote ambayo niliwahi kutaka kumuuliza, mengine nilipata majibu nlotaka na mengine yalitolewa mbavuni, kwa ki vyovyote vile nili enjoy sana mimi na wenzangu na kutoka kwetu tunatumai nawe uta enjoy kama ambayo nasi tuli enjoy na kujifunza kutoka kwa MWAMBA huyu. Love, Salama. --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support
More Episodes
Mfaume Mfaume ni yule mwana ambaye akitokea sehemu ni sahihi kwako kuwaambia wahusika kwamba jamani, mwamba huyu hapa! Muonekano wake pekee unamfanya mtu ajue yuko kwenye presence na mtu maalum na baadae ukishajua hasa nini anafanya basi huwezi ku doubt yote ambayo utaambiwa juu yake lakini kubwa...
Published 03/02/23
Published 03/02/23
Toufiq ni moja ya majina makubwa kati ya wafanya biashara wazuri na sasa mwanasiasa na Mbunge wa Mpendae, kwa wazee na vijana wa visiwani humo yeye ni mmoja wa mifano ya kuigwa ingawa kwake yeye yaliyo mengi kwenye maisha yake ni nguvu kubwa ilifanywa na Marehemu Mzee wake Ndugu Salih Hassan...
Published 02/23/23