SE7EP20 - SALAMA NA CAROL NDOSI | ANAMEREMETA
Listen now
Description
Ushawahi kuwa na mtu ambaye mnafahamiana vizuri miaka nenda na miaka rudi na hata pengine kwa u busy wa maisha zikapita siku hamjaongea lakini unajua yuko sawa yeye na Familia yake na mambo yanaenda vizuri, na kama isingekua hivyo basi ungekua ushajua? Ambaye unajua kukiwa na situation flani basi yeye anatafanya jambo flani na kuzima au kuwasha moto, na kama kuna neno umeambiwa kasema unajua kabisa ni kweli au si kweli? Au kama una suala unataka kulifahamu vizuri linalohusu mambo fulani na jibu ambalo atakupa yeye ni la 100 na hatapindisha hata kidogo? Basi huyo ni Carol Moses Ndosi kwa Salama Jabir yangu. Lini tulikutana? Yoh 😃! Wakati sote tunafanya kazi IPP Media,Carol alikua rafiki wa Tabea Kaduri ambaye alikua nae kwenye channel ya kiingereza ya 101.4. Si unamjua Carol na kizungu? Then ITV then EATV, mimi na Carol tukaja ku click zaidi kwasababu tabia zetu nyingi (za ujana) zinafanana. Pia tulienda wote Makongo Secondary School ingawa mimi huko simkumbuki maana mambo yangu yalikua mengi kiasi. Pia mimi ni Dada yake ki umri. Kuna story moja ya Carol ya kujifunza gari bila ya kunipa taarifa. Siku moja kaibuka tu ITV nje na kuniambia twenzetu kwa Kiula huku yeye ndo suka bila ya kujua lini hasa alijifunza kuendesha hilo gari! Nadhani hii ni moja ya memory nzuri kati yetu. Ukiachana na kwenda Chang’ombe kumfuata Steve Mbobo na gari letu ambalo AC Mungu ndo anajua,foleni ya Keko na sisi ilikua inafahamiana vizuri. Tumeishi na tunaendelea kuishi Alhamdulillah, na mambo yetu? Ah mambo yetu Allah anaendelea kuyabariki sana. Tunashkuru kwa kweli. Kukua sasa ndo huku, kila mmoja kajiajiri kwa kuyafanya yale aliyo jichagulia. Carol kama wengi mnao mfahamu na ambaye humu kwenye maongezi yetu ya kwenye kiti chakavu na meza ya kigae yatakufanya umfahamu zaidi kwamba ni JEMBE. Mpambanaji kabisa ambaye nae kama binadamu mwengine wakati mwengine humfika hhaapa na pengine kutaka kukata tamaa. Lakini uzuri ni kwamba ana nguvu na kiu ya kutaka KUENDELEA na KUSHINDA, pengine hiyo ndo silaha yake NAMBARI WANI. Kwa utashi wake ameweza na anaendelea kuweza kuwafunza mambo wengi wetu juu ya masuala ya ki mtandao na kujielewa binafsi. Wakati wa Nyama Choma Festival Carol na kikosi kazi chake aliweza kufanya kazi iliyo tukuka ambayo ililifanya tamasha hilo liwe ni moja ya matamasha BORA kabisa ambayo yashawahi kutokea hapa Tanzania. Mitihani ambayo aliwahi kukutana nayo wakati tamasha hilo likiwa linaendelea ambayo mengine ilikua ya Mungu na mengine ya Binadamu ni Carol mwenyewe na team yake ndo ambaye anaweza kuelezea na kwa kiasi kiduchu sana, amegusia kwenye maongezi haya. Heshima zangu kwake anazifahamu ingawa wakati mwengine tunakubaliana kuto kubaliana kwenye baadhi ya mambo lakini urafiki na u Ndugu wetu utabaki pale pale. Mimi na yeye tushafanya mengi, tushaona mengi, tushajifunza mengi na bado tunaendelea kufanya hivyo. Na nia hasa na madhumuni ya episode hii ilikua kutaka wewe unafahamu Ndugu yangu huyu zaidi. Na ningetamani sana kuweza kuyaweka wazi yooote na majina yake ila kwa staha na heshima, kwa leo tuishie hapa. Yangu matumaini kama kawaida utaokota mawili matatu ambayo yatakusaidia kwenye safari na vita zako binafsi. Keep going. Love, Salama. --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support
More Episodes
Mfaume Mfaume ni yule mwana ambaye akitokea sehemu ni sahihi kwako kuwaambia wahusika kwamba jamani, mwamba huyu hapa! Muonekano wake pekee unamfanya mtu ajue yuko kwenye presence na mtu maalum na baadae ukishajua hasa nini anafanya basi huwezi ku doubt yote ambayo utaambiwa juu yake lakini kubwa...
Published 03/02/23
Published 03/02/23
Toufiq ni moja ya majina makubwa kati ya wafanya biashara wazuri na sasa mwanasiasa na Mbunge wa Mpendae, kwa wazee na vijana wa visiwani humo yeye ni mmoja wa mifano ya kuigwa ingawa kwake yeye yaliyo mengi kwenye maisha yake ni nguvu kubwa ilifanywa na Marehemu Mzee wake Ndugu Salih Hassan...
Published 02/23/23