Episodes
Evarist Mapunda ni moja wa makocha wangu wa maisha haya ninayoishi sasa hivi, ananifahamu toka nikiwa na miaka 17 mpaka sasa hivi ingawa hapa katikati baada ya ‘kuwa mkubwa’ nilipoteana nae kwenye mahangaiko ya kujitafuta na kutafuta maisha. Ila Mimi na yeye tunajua kila mmoja wetu ni mtu wa aina gani na anamaanisha NINI kwa mwengine. Ukiwauliza watoto na wakubwa wengi wa Upanga watakuambia nini yeye pia anamaanisha kwenye maisha yao, lazima atakua na simulizi kuhusu mwalimu huyu hodari wa...
Published 09/15/22
Salum Mardhiya ni mmoja ya watu maarufu sana kwenye visiwa vya marashi ya karafuu yaani kule kwetu Zanzibar. Ni mmoja ya waalimu hodari anayeongoza kwa kutoa Da’wa kwa watu ambao wanasumbuliwa na matatizo mbali mbali. Kwenye nyumba karibu zote wanamfahamu maana huonekana mara kwa mara kwenye maeneo mbali mbali ili kusaidia wale ambao wanahitaji kisomo chake. Binafsi nilifahamiana nae kupitia rafiki ambae alinitambulisha kwake mapema mwaka huu, tena haikua imepangwa wala, alikuja sehemu ambayo...
Published 09/08/22
Tulia Ackson ni jina kubwa kati ya majina makubwa kwenye Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na kwa sisi kuweza kulipata jina kubwa na kukubali kuja kuketi kwenye kiti chetu chakavu ilikua ni BARAKA sana. Ila ukiachana na kwamba ni jina kubwa ila yeye ni binadamu, tena wa kawaida tu. Ni Mama, ni mke, ni Dada, ni Binti kwa Mama yake na ni Mbunge kwa wana Mbeya mjini lakini pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wadhifa ambao baada ya uchaguzi wa 2020 alirudi bungeni...
Published 09/01/22
Martin Kadinda ni rafiki yangu, ni moja ya wale wana ambao hana makuu na zaidi yeye anapeeenda sana kucheka, hata ukiangalia picha zake yeye ana tabasamu tu. Pengine hiyo ndo siri ya mafanikio yake tofauti yake na wengine na pengine hiyo ndo sababu ya mimi kumpenda sana. Pia ni FUNDI, tena mzuri tu sana. Kati ya mafundi wachache WAKWELI wa nchi hii Martin ni mmoja wapo, kama hawezi hawezi, hata siku moja hawezi chukua kazi yako alafu siku ya siku akakuharibia shughuli au mtoko. Kama yuko busy...
Published 08/25/22
Growing up kwenye mitaa ya Dar es Salaam na TV stations kali wakati huo zilikua na presenters makini na vijana ambao kwa kiasi kikubwa waliifanya tasnia hiyo ipendeze sana. Kuanzia vipindi vya watoto, vya muziki, filamu kutoka nje na tamthilia kutoka nje pia zilikua tamu sana, ukianza kuangalia TV kuanzia jioni hakuna mtu alikua anabanduka mpaka saa nne au tano za usiku, na kama ulikua jobless kama mimi enzi hizo basi ulikua unaunganisha na kuangalia marudio ya vipindi vya muziki ambavyo...
Published 08/18/22
Damian Soul ni Superstar na siku ambayo sote tutakubaliana na hiyo statement basi tutaanza kufaidi matunda ya kipaji chake kwa uzuri sana, ila mpaka siku hiyo ifike ni wachache tu ambao wanamuelewa kwa upana huo ndio ambao wataendelea kufaidi kipaji chake kwa nafasi yao. Wale watu wa makampunj mbali mbali kwa mfano CocaCola ambao wanakua na events zao za ndani kwaajili ya watu wao na waalikwa wawili watatu huwa wanamfaidi sana kijana huyu hodari wa ki Tanzania. Na Damian kwa ukali wake...
Published 08/11/22
Kila kijana wa ki Tanzania ambae anaupenda na kuuthamini mpira wa miguu na ambaye angependa ndo iwe kazi ya maisha yake basi Mbwana Ally Samatta ndiye role model wake, hakuna doubt kwamba watakua na mapenzi na Cristiano Ronaldo au Leo Messi au Kylian Mbappe au Marcus Rashford ila yule ambaye amewaaminisha kwamba INAWEZEKANA ukacheza POPOTE hapa duniani na hasa kwenye ligi yetu pendwa ya Uingereza ni Samatta. Rafiki tu kutoka Mbagala rangi tatu ambaye kashacheza saaana ndondo na makombe ya...
Published 08/04/22
Dr Kumbuka ni influencer mkubwa kwenye masuala ya mahusiano na maelewano inapokuja kwenye suala zima la ushauri na mashauri kwa watu wengi ambao wamekua wakimsikiliza na ambao wanamsikiliza kila siku za wiki anapokua kwenye kipindi cha Uhondo pale EFM. Na yeye kuwa pale hakufika kwa bahati mbaya. Ila pengine alipo anzia kazi yake pale Times FM ndo ilikua kama bahati kufika. Anakumbuka jinsi ambavyo alikua zake tu mtaani wakati mtangazaji wa Times FM wakati huo Bi Dida Shaibu alipokua mtaani...
Published 07/28/22
Ushawahi kukutana na wale watu ambao wao ni wa pole tu sana na wanajipenda tu sana ila hawana tu muda wa kuringa au kuji mwabafy kwasababu wao wako talented au wana kipawa kutoka kwa Allah na wanajua? Well mi nishawahi kukutana na watu kama hao na mmoja wao ni mgeni wetu RASMI wa wiki hii ya episode ya sita ya SalamaNa msimu huu. Anaongea kwa utaratibu na kujua kile atakacho, anakipataje na akisha kipata atafanya nacho nini. Huyo sasa ndo mwanangu Mtani Nyamakababi, aka Mtani Beskope. Kijana...
Published 07/21/22
Mwaka 2018 ndo nilimfahamu Oscar baada ya kukutana nae kwenye kituo changu cha kazi ya kutangaza mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika jijini Johannesburg nchini Afrika ya Kusini. Alikua mmoja ya watu ambao walinikaribisha vizuri sana kwenye team na kwa wakati huo yeye ndo alikua anaishikilia rekodi ya kuwa ndo mtangazaji mdogo zaidi kwenye team ya watangazaji nami nikaja kama Binti PEKEE ambaye ambaye alikua anatangaza mpira wa miguu kwa lugha ya Kiswahili. Combination yetu ilikua nzuri...
Published 07/14/22
Sheikh Hilali Shaweji Makarani au Sheikh Kipozeo ni mtu wa watu, au niseme kama ambavyo tunasema kwetu Uswazi, Sheikh ni mwana wa wana, anaweza kuwapa wana darsa kwa lugha yao na wakawa huru na wao kusema maoni yao au uelewa wao kwa raha na bashasha nyingi na naamini hii imemfanya yeye awe ni mmoja ya Ma Sheikh wanao tambulika zaidi kwenye mitandao ya kijamii nje na ndani ya Tanzania. Lugha hiyo ya wana ambayo anaitumia inasaidia sana kufikisha ujumbe ambao ameukusudia kwa wakati huo na...
Published 07/07/22
Abbot Charles ni jina maarufu kwa wanaoijua historia na wana zuoni, pengine umaarufu wa jina ndo sababu ya Baba yake kuamua kumpa mtoto wake wa kiume akitegemea na kijana wake atakua na ukubwa huo kwa lolote ambalo ataamua kufanya kwenye maisha yake, unaujua ule usemi kwa kiswahili kwamba maneno huumba? Mwenzangu, hata majina huumba, tena sana tu kwahiyo wakati mwengine utakapokua unafikiria jina la mwanao ni vyema kujiridhisha kwanza, unafanya kazi flani ya kipolisi ya kuchunguza ili mwanao...
Published 07/01/22
Kama kichwa cha habari kinavyosema, Engineer Hersi ndo chachu ya furaha kwa mashabiki wa moja ya timu kongwe kabisa ya Taifa hili, timu ya wananchi, timu yenye mataji mengi zaidi yaani mabingwa wa ki historia. Nikiwa kama shabiki wa Simba Sports Club basi sina la zaidi la kufanya ila kumpa mtani wangu Hongera ya kuongeza taji jengine kwenye historia yao na pia kumsifu round hii kwa kutuzuia kuchukua ubingwa kwa mara ya tano MFULULIZO.Engineer Hersi Ally Saidi aliingia pale kwa njia ya...
Published 06/23/22
Kuna usemi mmoja unaenda kama hivi, kulea mimba si kazi ila kazi ni kulea mtoto, tafsiri yangu naamini mhenga hapo alikua anatuambia kazi pengine inaanza baada ya kupata kazi, tunaelewa jinsi gani ambavyo kupata kazi huwa ni kazi. Tena kazi yoyote, haijalishi kama ni ya upishi au ulinzi au ufundi au hata u daktari, mi nawajua madaktari kadhaa ambao nao pia wanapata shida kupata hizo kazi. Na baada ya kupata shida zote hizo wakati wa kutafuta kazi basi kazi halisi huanza pale unapoipata sasa...
Published 06/16/22
SALAMA NA PROF JAY --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support
Published 02/25/21
Kutoka kwao Mbeya mpaka Dar es Salaam kwaajili ya kutafuta maisha bora na maendeleo kama wengi wetu ndo ilikua nia na madhumuni ya Raymond wa enzi hizo. Ingawa kuna kipindi ilifika alikua hataki kabisa kuskia habari za muziki, ila alipoambia kama kuna pesa ndani yake katika huo mchongo wa mashindano ambayo aliitiwa na akiangalia nyumbani moja haikai na mbili haijulikani ilipo akaona basi sawa, kwani nini? Na huo ndo ulikua mwanzo wa safari nzuri ya ki superstar ambayo anaishi nayo...
Published 02/18/21
Huyu si moja ya marafiki zangu, as in si Mtu amable nafahamiana naye sana, ambaye nishawahi kukaa naye muda mrefu na kupiga story, au kusafiri naye au kuwa studio wakati anafanya mambo yake au namjua mzazi wake au mtu wake wa karibu kwenye familia yake ila nawajua watu ambao wanamfahamu kwa ukaribu na watu hao ndo ambao walinipa mimi mawazo ya kutaka kumfahamu vizuri binti huyu hodari wa ki Tanzania bila ya hata ya wao kujua. Baadhi ya Dada zangu walifahamiana naye kwenye kipindi cha msiba...
Published 02/11/21
Haji Sunday Manara nlitaka kusema ni rafiki YANGU ila vacati navaza hilo nikakumbuka mmh, Haji Sunday Manara ni rafiki wa WATU WENGI hususan mashabiki wa klabu wangu pendwa na zaidi kwa watu ambao hawapendi hata mpira ila wanampenda tu jinsi anavyoseti mambo yake na anavyoigeuza sehemu yoyote aendayo kama sehemu yake ya kujitamba na kujitutumua na tofauti yake na WACHACHE ambao wanafanya kazi kama yake ni kwamba yeye anaweza KUYATEMBEA yale anayo YAONGEA. Mapenzi yangu kwake ni ya first...
Published 02/04/21
Hamis Tale Tale ni MWAMBA wa maisha yake na ya wale walomzunguka kwa miaka nenda miaka rudi na kutoka upande huu wa muandishi na mtangazaji ni heshima tu kwenda mbele. Kuna msemo mmoja wa Kiswahili kuhusu nyani ambaye unamkuta mjini. Ya kwamba anakua kashakwepa MISHALE ya kutosha kwahiyo unapomkuta town inabidi umpe heshima zake za kutosha. Kwa waasisi wa Bongo Flava jina lake kuwa juu pale na haiwezi kuwa kosa hata kidogo na kuna wasanii kibao ambao wana mshutumu kwa mambo mengi lakini kuna...
Published 01/30/21
Turudi nyuma mwaka 1999 wakati nilipomaliza kidato cha nne kwahiyo nilikua sina mitkasi mingi zaidi ya kumkimbia Mama inapofika mchana ili niende kucheza zangu basketball pale Msasani kiwanja cha Pazi. Nlikua natokea zangu Mbagala Charambe nachukua zangu basi mappa Mbagala Rangi tatu then muunganisho unaendelea mpaka nafika zangu mazoezini, nilifanya urafiki na makonda na madereva weeengi kiasi kwamba nilikua ‘staff’ kwenye daladala nyingi, na huwezi kuamini nyingi pia nilikua nikiingia basi...
Published 01/21/21
Kwa muda mrefu nimekua nikitaka kuongea na Mavoko ila ratiba zetu zilikua hazijawahi kuwa sawa na hivyo tukawa tunapishana tu. Kama mimi sina program naye basi yeye atakua free, na mimi nikiwa free basi yeye atakua na mipango ya kutoa kazi mpya ambayo itanifanya ningoje ili viende pamoja, au atakua kasafiri, au mimi nitakua nishaset watu wengine, ilikua kama tunacheza kidali po ila katikati ya mwezi wa kumi na mbili hatimaye yakatimia. Hakuna doubt juu ya uwezo wake popote pale utakapoenda...
Published 01/14/21
Muda si mrefu iliopita nilirudi nyuma kidogo kwenye kumbukumbu ya mawasiliano ya kwanza kabisa kati yangu na moja wa wasaidizi wake Mheshimiwa Jakaya Mrisho wa Kikwete na hiyo ilinirudisha nyuma mpaka mwezi wa tatu mwaka 2020. Kama mtu mwengine yoyote hii ilikua ndoto tu ambayo kwa Rehema na Baraka za Allah ilibidi itimie. Kwa Baraka zake hizo mimi na wenzangu tunashkuru sana sana kwa kuweza kulikamilisha hili. Shukran za dhati ziende kwa Doris Mollel ambaye kwa msaada wa Sadam ‘Almando’...
Published 01/07/21
Salama Na Joti --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support
Published 12/24/20
NJE YA BOX KIDDOGO --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support
Published 12/17/20
Pia anafahamkika kama Master T, mwenye sauti yake tamu ya kumfanya mtu abadilishe mawazo na kufanya anachosema yeye, lafdhi nzuri ya maneno ya Kiswahili na Kiingereza na tabasamu zuri kabisa lililokaa mahala pake na hiyo ndo tofauti ya Taji Liundi na watangazaji pamoja na hata viongozi wa department mbali mbali kwenye vyombo vyetu vya habari vya ‘siku hizi’. Taji alibahatika kuzaliwa kwenye familia yenye uwezo kwa kiasi chake na malezi bora aliyapata kwa Baba yake ambaye muda mwingi alikua...
Published 12/11/20