SE7EP16 - SALAMA NA ZAHIR ZORRO | KIMULIMULI
Listen now
Description
Zahir Ally Zorro ni mkongwe wa muziki wa dansi na kwa habari ambazo nimepata ni kwamba enzi zake alikua wa moooto sana tena kwenye kila nyanja, kuimba, kuandika, kupiga gitaa na mpaka uvaaji, alikua handsome boy sana na ulimbo kwa kina Dada enzi hizo. Utashi na ucheshi na u sharp wake ndo ambao ulikua unamfanya asimame PEKEE kwenye kadamnasi ya wanamuziki wengi wa kipindi hiko. Naomba nikukumbushe pia kwamba enzi hizo zilikua pia si za kuzichukulia poa kabisa, maana ushindani wa bendi na vipaji binafsi ulikua wa hali ya juu sana, na yeye kama yeye alikua moja ya wale WAKALI wa kipindi hiko. Kama muajiriwa wa Jeshi Mzee Zahir alikua shujaa wa aina yake enzi hizo za ujana wake, kama askari alikua akijituma na ndo maana hakua na cheo cha kinyonge, na kama muandishi na muimbaji na mpiga gitaa pia alikua na nafasi yake ya kipekee. Ukimuangalia hata rangi yake imekaa ki chotara na kwenye mazungumzo haya ana nikumbushia jinsi ambavyo Baba na Mama yake walikutana na ambavyo yeye alizaliwa. Interest yangu zaidi ilikua jinsi ambavyo yeye kama Baba ameweza kuwakuza watoto wake wawili ambao nao wamekuja kuwa wanamuziki wazuri tu tena, Marehemu Maunda Zorro ambaye alifariki mapema mwaka huu (Mwenyezi Mungu amsamehe makosa yake na Amrehemu) na Kaka yake Banana Zorro. Wakati wa kuanza Banana ndo alionekana kuwa angekua super star zaidi ila Maunda nae alipoikamata reli yake kila mtu alimfahamu vizuri. Malezi yao baada ya Marehemu Mama yao nae kutangulia mbele ya haki wakiwa bado wadogo naamini ilikua mtihani mkubwa kwa Mzee Zorro. Ila kwa Rehema za Mwenyezi Mungu Mzee huyo aliweza na ameweza kuhakikisha watoto wake wanakaa kwenye mstari ulio nyooka na kufanya mziki mzuri na kwa heshima na taadhima. Kwenye maisha yangu ya kazi hii nimeshawahi kukutana na Mzee Zorro ila hatukuwahi kufanya maongezi kama haya ingawa nyuma ya ubongo wangu siku zote nilikua nataka kufanya hivyo, na wakati mwengine nilikua nawaza hata ingekua viti VITATU upande ule yaani Baba na watoto wake wawili, kisha nikaona tutakosa kinaga ubaga nyingi, yaani hatutawafaidi sana kama tukiamua kufanya hivyo maana kati ya watatu hao kila mmoja ana story zake ambazo anafaa kupatiwa wasaa wake. Kwa bahati mbaya Maunda alitangulia mbele ya haki na wakati kwa upande wetu ulifika kwa sisi kutaka kukaa chini na Mzee Zorro ili tuyajue yake na kutaka kujifunza kutoka kwake. Mimi na Director wangu wa episode hii tulikua na wakati mgumu kiasi maana pengine tulitaka zaidi ya ambacho tuliweza kupata na hilo Mimi na Alex (Director wangu) tumekubaliana kwamba imetokana na kuondoka kwa Maunda, tunaamini toka Maunda amefariki Mzee Zorro hajarudi katika hali yake ya kawaida, na inaeleweka maana yule hakua tu Binti yake, alikua ni rafiki yake wa karibi saaaana pia. Mzee Zahir alikua analala na Maunda na Banana chumba kimoja mpaka siku chachu tu kabla ya Maunda kukua, na hiyo ilikuja baada ya Banana kumuambia Mzee wake kwamba pengine sasa umefika muda wa wao kulala tofauti. Ananiambia katika episode hii kwamba yeye waala hakua anaona tatizo lolote juu ya hilo maana wenyewe walikua wanaishi tu kwa upendo na maelewano ila baada sasa ya Banana kusema ndo hata yeye alipoona ni kweli muda wa kupeana faragha kwa kila mmoja kuwa na sehemu yake ulikua ushafika. Kwa mtu ambaye walikua wanaonana karibu kila siku na kuongea sana hata baada ya Maunda kuhamia kwa mtu wake ukaribu wao bado ulikua wa karibu sana. Mimi namuombea Mzee Zahir Ally Zorro wepesi katika kipindi hiki kigumu ambacho anapitia na In Shaa Allah arudi katika hali yake ya zamani ya ucheshi na bashasha tele na kwa hii ambayo tumeweza kufanya naye itakupa ufahamu wa kiasi wa legend huyu ambaye pia ni mjuzi wa mambo mengi ya historia na muziki wa jana na wa leo hapa ulimwenguni, ukitaka kuongea na Mzee Zorro hukusu culture ya Mexico, mabadiliko ya tabia nchi, timu ya Taifa ya Ufaransa, mapenzi ya Tabu Ley na Mbilia Bel yote atakua na la kukuambia. Special special human being. Tafadhali enjoy.  Love, Salama.   --- Support this podcast:
More Episodes
Mfaume Mfaume ni yule mwana ambaye akitokea sehemu ni sahihi kwako kuwaambia wahusika kwamba jamani, mwamba huyu hapa! Muonekano wake pekee unamfanya mtu ajue yuko kwenye presence na mtu maalum na baadae ukishajua hasa nini anafanya basi huwezi ku doubt yote ambayo utaambiwa juu yake lakini kubwa...
Published 03/02/23
Published 03/02/23
Toufiq ni moja ya majina makubwa kati ya wafanya biashara wazuri na sasa mwanasiasa na Mbunge wa Mpendae, kwa wazee na vijana wa visiwani humo yeye ni mmoja wa mifano ya kuigwa ingawa kwake yeye yaliyo mengi kwenye maisha yake ni nguvu kubwa ilifanywa na Marehemu Mzee wake Ndugu Salih Hassan...
Published 02/23/23