SE7EP15 - SALAMA NA MCHUNGAJI RICH BILIONEA | SERMON
Listen now
Description
Kipindi cha nyuma kidogo nilifanya lile ambalo huwa nafanya la kuwashirikisha rafiki zangu na team kuhusu list ya watu ambao wangependa kuwaona kwenye kiti chetu chakavu na sababu za kwanini hasa waje kwenye meza ile yenye kigae kwa juu maana tukisema tutaje majina tu bila ya sababu thabit za wao kuja pale tunaweza tukaondoa maana yenyewe ya kuwa na watu wenye story za kuvutia na kutufunza kama ambavyo tumekua tukifanya. Jina la mgeni wetu huyu lililetwa kwangu na Michael (Mx) Mlingwa na Ndugu yangu Elbogast Myaluko ndo alinipatia mawasiliano naye na kuanzia hapo mengine yamebaki kukhadithiwa kama hivi. Sikua namfahamu Mchungaji Richard Hananja mpaka Michael alipo niambia nami nikachukua muda wangu wa kwenda kufanya ka research kangu kabla hajaja mezani, ambacho nilijifunza ni kwamba Mchungaji alikua ni mtu mashuhuri sana ambaye ana watu wengi sana pia wanao mskiliza. Ilinichukua takriban miezi miwili kuweza kumpata maana kila weekend (mara nyingi rekodi za kipindi huwa zinafanyika weekend) yeye huwa yuko safarini. Huitwa sana sehemu mbali mbali, na sasa Serikali nayo imekua ikimuita pia katika matamasha na mikutano mbalimbali. Kwahiyo mara utamsikia yuko Dodoma, mara Moshi, mara Iringa ilimradi yuko busy. Na wakati mwengine Jumapili yake inakua ya yeye kualikwa kwenye Makanisa mbalimbali ili akatoe neno, siku hizi yeye ameshastaafu kuhubiri kanisani na sasa zilizobaki ni hizo za mialiko maalum. Kama kawaida mimi na wenzangu tulitaka kuanza kwa kumfahamu mgeni wetu maana kama nilivyokuambia hapo awali mimi sikua namfahamu zaidi tu ya kumuona kwenye mitandao akimwaga cheche, tulianzia kwenye kuzaliwa kwake na kukua kwake, mitihani mbalimbali ya ujana, bishara na kazi ambazo ashawahi fanya, na wakati naandika hii nimejifunza pia kuwa Mchungaji hana ambalo anaongeza chumvi maana baada ya sisi kufanya nae maongezi haya, nimeona ameenda sehemu tofauti tofauti na story yake haijawahi kubadilika. Ujasiri wa ziada huhitajika ili tuweze kufanikiwa kwenye maisha yetu na pia kuwa kwenye mstari ili usiingie kwenye matatizo na vyombo vya sheria. Mchungaji ananiambia jinsi ambavyo alikua ana hustle kila kona, kusafiri bila ya kibali cha kuvuka mipaka ya nchi na boxing ambayo aliifanya kwenye kipindi flani kwenye maisha yake. Boxing imemuachia kovu ambalo kila siku linamkubusha mapambano ambayo ameshawahi kuyafanya kwenye maisha yake. Boxing pia ndo ambayo imemfanya awe na discipline ya hali ya juu. Kwenye maisha yake ya sasa Mchungaji Hananja anatoa nafasi kwa kila aliye kata tamaa au ambae watu wamemkatia tamaa, yeye ndo huwachukua hao na kuwapa nafasi nyengine kwenye maisha yao, na amini usiamini wengi wao hunyooka na kuanza upya. Kwenye nyumba yake huko Madale Mchungaji anafanya mambo mengi ikiwa pamoja na kilimo na ufugaji. Swali langu lilianza kwa kutaka kujua hizo pesa za yeye kuweza kufanya mambo yote hayo, huwa zinatoka wapi? Mchungaji Hananja ni MUME, na kwa mujibu wa maelezo yake, alichelewa saana kuoa na mkewe ni Rafiki yake wa kwanza. Yangu matumaini moja mbili tulizopiga humu zitakupeleka sehemu. Tafadhali enjoy. Love, Salama. --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support
More Episodes
Mfaume Mfaume ni yule mwana ambaye akitokea sehemu ni sahihi kwako kuwaambia wahusika kwamba jamani, mwamba huyu hapa! Muonekano wake pekee unamfanya mtu ajue yuko kwenye presence na mtu maalum na baadae ukishajua hasa nini anafanya basi huwezi ku doubt yote ambayo utaambiwa juu yake lakini kubwa...
Published 03/02/23
Published 03/02/23
Toufiq ni moja ya majina makubwa kati ya wafanya biashara wazuri na sasa mwanasiasa na Mbunge wa Mpendae, kwa wazee na vijana wa visiwani humo yeye ni mmoja wa mifano ya kuigwa ingawa kwake yeye yaliyo mengi kwenye maisha yake ni nguvu kubwa ilifanywa na Marehemu Mzee wake Ndugu Salih Hassan...
Published 02/23/23