SE7EP19 - SALAMA NA DITTO | TUNER
Listen now
Description
Lameck Ditto Sr ni Baba, Mwalimu, mwanamuziki, muandishi, mentor, mume na zaidi ya yote ni mwana tu ambaye maisha alopitoa kipindi anakua hayajawahi na wala hayatawahi kumsahaulisha yeye ni nani na wapi ambapo ametokea na wapi anataka sana kuelekea maana huko ndo kwenye kesho yake, na kwa kumsikiliza ambavyo nimemsikiliza, kesho yake anaithamini sana na amekua akiiandaa vizuri ili hata siku moja asije akakwama na kuanza kuishi maisha ya jana ambayo yalikua si mazuri hata kidogo. Yeye na Baba yake mzazi walikutana kwa ‘bahati mbaya’ tunaweza tukasema hivyo maana wakati yuko zake Morogoro akiendelea na maisha ya kuishi yeye na Kulwa huku wakijilea wenyewe, Ditto au Dotto ananihadithia vile ambavyo Rafiki yake aliweza kumkutanisha na Mzee wake bila ya yeye kutegemea. Alikua ananiambia vile ambayo ilikua inabidi apambane kupata ya kula na pa kulala baada ya kuja jijini Dar es Salaam na haya yote ni baada ya yeye tayari kuwa umeshatoka na WATU PORI enzi hizo na hapo pia ni baada ya kupata nafasi ya kurekodi album moja na producer PFunk enzi hizo, PFunk huyo huyo ambaye alikua akilitikisa TAIFA kwa kazi nzuuri alizokua akifanya na wasanii kadha wa kadha ikiwa pamoja na Juma Nature. Lameck anakumbuka jinsi alivyokua analala ndani ya kiduka kidogo cha mwanawe mmoja ambaye alishamsomesha ili amstiri ki hivyo, alivyokuja Dar alikua anakaa kwa mwanae mmoja ivi na mkewe ila baada ya ahadi za album kutoka na kwamba mambo yatabadilika kugonga mwamba, Lameck ilibidi atafute ustaraabu mwengine. Nilitaka kujua kama hiyo ndo ilikua lowest moment ya maisha yake? Au kifo cha Mama yake? Au Mamu kukataa album yake kwa kusema haikua na kiwango kile? Sasa ni Baba na mchumba wa muda mrefu wa Binti mmoja ambaye nae alikutana nae ki ajabu ajabu tu na ambaye pia alimzungusha sana kabla hajanasa kwenye ndoana. Baba wa mtoto ambaye Mimi baada ya kukufanya nae mazungumzo nilikutana nae uwanjani akiwa ameenda kumuangalia Lameck Jr akifanya yake kwenye moja ya mechi za soka za shule ambayo anasoma. Kwenye meza aliniambia moja ya ahadi ambazo amejiwekea ni kuhakikisha yuko pale kwaajili ya mtoto wake, jambo ambalo yeye hakuwahi kulipata mapema. Mwanzo nilikuambia yeye pia ni muandishi, muandishi wa mashairi ya muziki na pia ni muandishi wa matangazo, kazi ambayo anasema Marehemu Ruge Mutahaba ndiye ambaye kwa kiasi kikubwa alimuelekezea huko. Na mentor wake mwengine ni Ndugu Ruben Ncha Kalih ambaye kwa asilimia KUBWA amempika na akapikika. Tulizungumzia pia umuhimu wa mmoja kuwa na chanzo zaidi ya kimoja cha kupata pesa, kuweza kukabiliana na MSIMU ambao unakua huna wimbo (au kazi) lakini bado ukaweza kuishi, kuhusu maamuzi ya yeye kwenda THT wakati tayari alikua ARTIST ambaye ameshajijenga. Tuliongea pia kuhusu Ruge, Barnaba, Amini na mambo mengine tele. Binafsi nilikua na wakati mzuri sana wakati tunaongea haya na yangu matumaini itakua hivyo kwako pia. Tafadhali enjoy. Love, Salama. --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support
More Episodes
Mfaume Mfaume ni yule mwana ambaye akitokea sehemu ni sahihi kwako kuwaambia wahusika kwamba jamani, mwamba huyu hapa! Muonekano wake pekee unamfanya mtu ajue yuko kwenye presence na mtu maalum na baadae ukishajua hasa nini anafanya basi huwezi ku doubt yote ambayo utaambiwa juu yake lakini kubwa...
Published 03/02/23
Published 03/02/23
Toufiq ni moja ya majina makubwa kati ya wafanya biashara wazuri na sasa mwanasiasa na Mbunge wa Mpendae, kwa wazee na vijana wa visiwani humo yeye ni mmoja wa mifano ya kuigwa ingawa kwake yeye yaliyo mengi kwenye maisha yake ni nguvu kubwa ilifanywa na Marehemu Mzee wake Ndugu Salih Hassan...
Published 02/23/23