SE7EP18 - SALAMA NA FAROUK KAREEM | SAILOR
Listen now
Description
Hii nayo ni moja ya zile ambazo ziliuliziwa sana na kwa muda mrefu nasi kwa upande wetu tumekua tukiifukuzia tuweze kukaa na mwamba huyu hodari kutoka Zanzibar. Mimi mwenyewe ambaye nimekua nikifanya kazi kwenye kiwanda hiki cha burudani nilikua na hamu ya siku moja kuwa kwenye meza moja na Ndugu yangu huyu, kuweza kumtazama usoni na kumuuliza yote ambayo nilikua nataka kumuuliza kwa kipindi kirefu sana. Maana hata mimi nimekua nikimsikiliza miaka nenda miaka rudi na siku zote emeemdelea kutuhabarisha kwa sauti ile ile na spidi ile ile. Ukiskia mtu ameweza kuwa bora toka siku ya kwanza basi moja ya mifano hai ni Farouk Kareem wa ITV na Radio One. Nikiwa mzanzibari wa kuzaliwa, Farouk amekua ni moja ya watu ambao nimekua nikiwaskiliza na kuwaheshimu sana. Mchango wake kwenye tasnia ya uwandishi wa habari na kuziripoti habari hizo Taifa zima unalijua, toka enzi zile za kipindi cha Spoti Leo cha Radio One ambacho yeye alikua alishiriki kama reporter kutoka Zanzibar na baadae na yeye akajiingiza katika kinyang’anyiro cha kugombea nafasi ya uongozi kwenye Chama cha Mpira cha Zanzibar yaani ZFA na akapata na katika watu ambao walipiga kazi iliyo TUKUKA enzi hizo na ambayo iliacha alama basi Farouk ni mmoja wapo. Nani aatasahau kama moja ya idea zake ilikua ile ya kutaka Zanzibar iwe na kiti chake kwenye Shirika la Mpira la Afrika na la Dunia yaani CEFAFA na FIFA. Farouk Kareem alikua ndo injinia wa kutaka hilo LIWEZEKANE. Mtoto wa kwanza kwenye familia ya watoto wawili tu na wote wa kiume, Farouk Karim ni Kaka wa mmoja kati ya ma Pilot hodari na wa muda mrefu ambao hii nchi imeshawahi kuona ambaye na yeye sasa ana mtoto pia ambaye naye ni Rubani. Kaka huyo Kapten Arif Jinnah na mwanawe First Officer Amour Arif. Ki ufupi familia yao imejaa watu wa kazi kabisa. Naamini si wengi ambao tulikua tunayajua mahusiano hayo ya wawili hawa ambao kila mmoja wao amekua akiandika historia yake kwa upande wake. Farouk ni Baba wa watoto kadhaa wa Kike ila miaka si mingi sana Allah pia nae kampa mtoto wa kiume. Kwenye episode hii tumezungumzia familia na majukumu, tumezungumzia jinsi mmoja anavyoweza kutafuta kwa njia zake na wazazi nao wakitoa baraka zao basi hakuna ambalo linaweza kushindikana kama tu nia na madhumuni yapo. Anakumbuka jinsi ambavyo alimaliza skuli na kisha akawaambia wazazi wake kwamba yeye anataka kuwa BAHARIA na wao WAKARIDHIA. Anasema kipindi hiko kulikua na wimbi la ma Seaman tele ambao walikua wakirudi likizo nyumbani Zanzibar wanakua wako ‘vizuri sana’ na hiyo ni moja ya mambo ambayo yalimvutia sana. Na wazazi wake waliridhia na kuhakikisha kijana wao anatimiza ndoto zake kwa kumuwezesha. So, kwenye habari nako alifikaje? Hii ni moja ya episode nzuri sana ambazo nimewahi kufanya msimu huu na yangu matumaini nawe uta enjoy kama ambavyo sisi tuliburudika wakati wa mahojioani haya.  Love,  Salama. --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support
More Episodes
Mfaume Mfaume ni yule mwana ambaye akitokea sehemu ni sahihi kwako kuwaambia wahusika kwamba jamani, mwamba huyu hapa! Muonekano wake pekee unamfanya mtu ajue yuko kwenye presence na mtu maalum na baadae ukishajua hasa nini anafanya basi huwezi ku doubt yote ambayo utaambiwa juu yake lakini kubwa...
Published 03/02/23
Published 03/02/23
Toufiq ni moja ya majina makubwa kati ya wafanya biashara wazuri na sasa mwanasiasa na Mbunge wa Mpendae, kwa wazee na vijana wa visiwani humo yeye ni mmoja wa mifano ya kuigwa ingawa kwake yeye yaliyo mengi kwenye maisha yake ni nguvu kubwa ilifanywa na Marehemu Mzee wake Ndugu Salih Hassan...
Published 02/23/23