SE7EP23 - SALAMA NA WALTER CHILAMBO | HABA NA HABA
Listen now
Description
Pengine jina la episode hii linaweza likakupa muangaza kidogo wa story fupi ya maisha ya mgeni wetu wa wiki hii kwenye kiti chetu chakavu na meza ya kigae ambaye leo hii tayari kashaona, tochi ya maisha kwake inamulika tu vizuri na mbele anapaona. Huyu ni Walter Chilambo ambaye miaka tuseme 14 iliyopita alikua hana uhakika wa chakula chake cha siku tu achana na sehemu gani atalala. Ruka ruka ya kule na huku na bahati ya kupendwa alonayo na ambayo inaendelea mpaka leo naamini inakuja kwasababu ya ukarimu wake na hii ndo silaha yake yenye makali ambayo inampeleka mbali mpaka leo hii. Kama mtoto wa kiume ambaye unatakiwa kwenda kujitafuta ki maisha Walter nae ilibidi afanye yale yale ambayo si watoto wa kiume tu ila wengi wetu tumefanya ya kutaka kwenda kutafuta chako, na yeye aliona basi bora afanye hivyo. Safari ya kuja town kutoka mkoani anatuhadithia kwa upana kwenye episode hii. Mtu ambaye alimpokea ni mwana tu ambaye alienda nae shule moja, stop ya kwanza? Keko Magurumbasi. Na si kwamba alikua hana Ndugu hapa Dar es Salaam yeye alijiamulia isiwe hivyo, ilikua ngumu kumshashiwi Mama yake ambaye alitaka kujua ramani nzima ya mwanae ambaye alikua anakuja mjini kwa mara ya kwanza. Baada ya kufanikiwa kushawishi Mama Walter, kijana alipewa nauli na ananiambia by the time anafika Dar alikua na shilingi ELFU MOJA TU kwenye mfuko wake, hapo ni Ubungo kwenye stendi ya mkoa. Imani yake kwa Mungu wake pia ni silaha ya pili ya Ndugu Walter Chilambo. Hii ndo ambayo kwa mujibu wake imemsaidia kumvusha na mengi, maisha huko Keko hayakua mazuri, sikutaka kutumia neno si kama alivyo yatarajia maana hata yeye hakua na matarajio yoyote kwasababu alikua hajui anakutana na mazingira gani wakati anaenda kwa mwanae huyu aliyesoma nae Sekondari ambaye walikua na majina ya Baba yanayofanana. Mwenzetu anaitwa Michael. Alikaa pale huku akiwa anajaribu kuji tafuta ila kila anachogusa kilikua cha moto. Ananihadithia jinsi alivyoanza kufanya kazi za kila siku ili angalau apate hela ya kula, kule kwa Mama alikua anajifanya kama kila kitu kinaenda vizuri kwahiyo hata vimzinga vidogo vidogo vilikua haviendi. Ulipofika wakati wa yeye na mwanae Michael kufunguana mashati maana alikua ashakaa saana na hana dira nzuri hapo sasa ndo kila kitu kilianzia. Unadhani mmoja anaweza kuwa na bahati kiasi gani kwamba mtu ambaye aliombwa amhifadhi kwenye ghetto lake wakati yeye anatafuta ustaarabu mwengine kuwa ni Ndugu yake? Pengine hii hutokea kwa wenye BAHATI TU, pengine Walter ni mmoja ya watu hao maana baada ya kujulikana hilo ndo angalau kukawa na ahueni ya kuwa na uhakika wa sehemu ya kuegesha mbavu, hii ni moja ya sehemu ilonisisimua kwenye simulizi yake, imagine mtu anavyokua kapigika alafu kutoka ambako hakujulikani mtu ambaye ameombwa akuhifadhi kwa muda anatokea kuwa ni Ndugu yako, hii ni Mwenyezi Mungu pekee ndo ambaye anaweza KUTENDA na kama utakua ushawahi kuishi kama ndege ambaye hajui analala wapi basi wewe utaweza kuelewa zaidi hapa. Walter Chilambo ni mshindi wa Bongo Star Search wa mwaka 2012 na baada ya kushinda alianza safari yake ya muziki rasmi. Safari yake haikua ya urahisi kama ambavyo naamini alitarajia au sote tulidhani. Kiwanda cha Bongo Flava ki usalama tunaweza kusema kina wenyewe na ukiwa mpya kabla hujajua fagio lipi ndo linafaa kusafishia wapi basi kazi utakua nayo. Kwa Bwana Chilambo ambaye alishinda taji na pesa hakukua na tofauti kabisa. Neema kwa upande wake ilianza kuonekana baada ya yeye kuamua kufanya mziki wa kumtukuza Mungu na baada ya hapo mengine ni story tu. Kwahiyo NINI hasa kilimfanya afanye maamuzi hayo? Kwenye kipindi ambacho kila mmoja ameamua kuimba nyimbo za mambo ya kitandani na mambo ya ndani je yeye kwanini aliamua kubadilisha gea? Maana Kama sauti anayo na kuandika anajua sasa sababu ni nini? Na pia wasiwasi wangu uko kwenye baada ya ‘kutoboa’ huko aliko na kupata umaarufu na sifa tele hatorudi tena huku kwenye kuimba nyimbo za kuachwa na kupendwa na kutendwa? Ana uhakika kiasi gani? Ukichukulia kama k
More Episodes
Mfaume Mfaume ni yule mwana ambaye akitokea sehemu ni sahihi kwako kuwaambia wahusika kwamba jamani, mwamba huyu hapa! Muonekano wake pekee unamfanya mtu ajue yuko kwenye presence na mtu maalum na baadae ukishajua hasa nini anafanya basi huwezi ku doubt yote ambayo utaambiwa juu yake lakini kubwa...
Published 03/02/23
Published 03/02/23
Toufiq ni moja ya majina makubwa kati ya wafanya biashara wazuri na sasa mwanasiasa na Mbunge wa Mpendae, kwa wazee na vijana wa visiwani humo yeye ni mmoja wa mifano ya kuigwa ingawa kwake yeye yaliyo mengi kwenye maisha yake ni nguvu kubwa ilifanywa na Marehemu Mzee wake Ndugu Salih Hassan...
Published 02/23/23