Description
Mrisho Halfani Ngassa alikua top top top footballer na kwa bahati nzuri nishawahi kumshuhudia akiwa kazini kwake, tena ukimkuta kaamka vizuri basi uhakika wa burudani ni UHAKIKA . Na kipindi ambacho alikua kwenye peak yake pia kulikua na vitasa imara na magolkipa wazuri tu lakini nna uhakika kila mmoja kati yao ana la kusema kuhusu winga na forward hii machachari ambayo nchi yetu ishawahi kuona. Hakuna kitasa ambacho hakijawahi kukataa kufungua mlango muda ambao Mrisho Ngassa alikua anakuja kupiga hodi.
Uzuri wake alianza kucheza mapema sana na kwasababu alikua machachari basi hata utulivu kidogo wakati anakua ulikua sio mzuri sana maana alikua na haraka. Ananiambia kwenye session hii vile ambavyo ali sign Yanga pasi na kumskiliza kocha wake kutoka Mwanza ambaye alikua anaamini kama dogo bado hajaiva, Pengine miaka miwili au mitatu ya kuendelea kujijenga ingemfanya awe bora zaidi na zaidi lakini kwenye kichwa na fikra za kijana huyu ambaye alikua na uchu wa mafanikio na kutaka kufika mjini maongezi hayo ya kusubiri yalikua ni kama kumuona sisimizi kwenye sukari alafu unamuambia asile leo badala yake ataila asubuhi, isingewezekana. Hivyo kocha akaona basi si mbaya, aende akayaone na kujifunza akiwa kazini.
Yanga ndo Yanga, kwa wachezaji wote wanao chipukia au ambao ndo wanatafuta maisha kuichezea klabu kama ya wananchi ni heshima kubwa sana na zaidi kama wao ndo wametaka iwe hivyo. Kwa kijana mdogo ambaye alikua na spidi na uchu mkubwa wa kuzitia nyavuni basi klabuni pale ndo ilikua steji muafaka ya kuonyesha kipaji chake. Mrisho anakumbuka aina ya ‘vifaa’ ambavyo vilikua vinapatikana mitaa ya Jangwani. Majina makubwa na kazi ilotukuka ambayo walikua wakiifanya ilikua inajielezea. Kwa kijana kutoka mkoani kuweza kupata namba haikua kazi rahisi, ila pia haikua kazi ngumu maana ulichokisia ndo ambacho unakiona, kuanzia mazoezini mpaka anapopatiwa nafasi wakati wa mechi.
Kwenye episode hii tunazungumzia aina ya mitihani na maamuzi ambayo ilikua inabidi yafanyike. Kwenye wasifu wake Mrisho amewahi kucheza kwenye team zote tatu kubwa hapa nyumbani kwetu. Kashawahi kuwa muajiriwa wa Yanga, Azam na Simba ambapo alienda kwa mkopo kutoka Azam FC, lakini pia ashawahi kupatiwa majaribio katika team kadhaa nje ya nchi yetu na wakubwa wanasema kama Ndugu yetu angekua katuliza akili na angefahamu aina ya nafasi ambayo alikua nayo kipindi kile basi yeye ndo angekua mtanzania wa kwanza kucheza kwenye ligi pendwa ya Uingereza. Trials kwenye klabu kama Westham alipata na ofa kwenye vilabu kadhaa kutoka hapa hapa barani Afrika nazo zilikua hazikati.
Sasa, nini haswa kilitokea? Wapi hasa alienda mrama? Ni kweli alikosea? Au malengo yake si malengo yetu? Au tulipokua tunamuona sisi yeye alikua hapaoni huko? Vikwazo vilikua nini? Mambo yepi hasa ndo ambayo yanaweza yakawa ndo chachu ya hayo yote kutotokea? Kama Mrisho angekua anawez kufunguka zaidi nami kwenye episode hii naamini tungeweza kupata funzo lilonyooka kwa wenetu na ukichukulia sasa mambo ndo yameanza kufunguka. Naamini angekua mwalimu mzuri kwa wake wote ambao wangetaka kusoma somo ambalo lina uhitaji mkubwa.
Yangu matumaini utaweza kuelewa na kupata chochote kitu kutoka kwenye maongezi haya.
Tafadhali enjoy.
Love,
Salama.
---
Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support
Mfaume Mfaume ni yule mwana ambaye akitokea sehemu ni sahihi kwako kuwaambia wahusika kwamba jamani, mwamba huyu hapa! Muonekano wake pekee unamfanya mtu ajue yuko kwenye presence na mtu maalum na baadae ukishajua hasa nini anafanya basi huwezi ku doubt yote ambayo utaambiwa juu yake lakini kubwa...
Published 03/02/23
Toufiq ni moja ya majina makubwa kati ya wafanya biashara wazuri na sasa mwanasiasa na Mbunge wa Mpendae, kwa wazee na vijana wa visiwani humo yeye ni mmoja wa mifano ya kuigwa ingawa kwake yeye yaliyo mengi kwenye maisha yake ni nguvu kubwa ilifanywa na Marehemu Mzee wake Ndugu Salih Hassan...
Published 02/23/23