SE7EP25 - SALAMA NA DORIS MOLLEL | HALF WOMAN, HALF AMAZING
Listen now
Description
Doris Mollel kwa kuanzia tu tuanze na jina lake, ni zuri lenye kukumbukwa ki rahisi, yeye mwenyewe pia ni mrembo na mkarimu, sana. Roho yake ni kama rangi yake, nyeupe na kwa bahati Mimi namfahamu yeye kiasi kwa kupitia rafiki zangu ambao yeye anafanya nao kazi na pia ana mahusiano nao mazuri, sana. Pia namfahamu mume wake ambaye tukianza shindano la kumtafuta nani mkarimu kati yao tunaweza kukamaliza kwa suluhu. Huwa naamini Mwenyezi aliwakutanisha ili kwa pamoja waweze kufanya makubwa kwaajili yao na familia zao na jamii ambayo imewanzunguka ambayo kwa kiasi kikubwa ina uhitaji wa yale ambayo wao wameyaona wanaweza kufanya jambo ili yawe mepesi. Sasa tuanze kwa vipi Doris amekua akifanya ambayo anayafanya sasa ambayo baada ya kufanya kipindi hiki mengi ambayo aliyaongelea kama ya Serikali ya Uganda kumpa tuzo na kumkaribisha nchini mwao ili aweze kushirikiana nao bega kwa bega kwenye suala zima la kuwaokoa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati yaani ‘NJITI’ na hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia S. Hassan kutoa MILIONI 70 kwaajili ya kuchangia mfuko wake wa Doris Mollel Foundation. Yeye alikua anataka tu kufanya kitu kwaajili ya kuisadia jamii yake, ananiambia wakati analizungumzia hilo huku akitafuta jambo la kufanya ndipo Mama yake alipomfugua macho kwa kumuambia masuala ya watoto njiti, taa iliwaka sasa baada ya Mama yake kumkumbusha kwamba hata yeye alizaliwa kabla ya wakati. Alipoambiwa hivyo hakukua na kurudi nyuma tena baada ya hapo. Ananisimulia vikwazo ambayo aliwahi kupata mwanzo kuanzia nyumbani mpaka kwenye kutafuta hizo pesa ambazo zinasaidia mpaka leo hii, Doris ananihadithia jinsi ambavyo alipata bahati ya kuwa na watu ambao wamemsapoti na wanamsapoti mpaka leo kuanzia nyumbani kwa mume wake. Mtu ambae ndoa yao ilikua changa kuanza kuwa na vikao na watu mbali mbali mpaka usiku wa manane inamtaka mtu muelewa sana kuweza kuamini na kuyaacha mambo yaende. Mumewe alikua huyo mtu. Kwa ambao walimpigia simu mara ya kwanza baada ya kuona anchojaribu kufanya, watu kama Asas wa kule Iringa na wengine ambao wamekua wakijitokeza siku baada ya siku. Anakumbuka na anajua kwamba kutokata tamaa kwasababu ya changamoto kadhaa ndo ambapo kunamfanya awe ni mmoja ya watu wanao heshimika zaidi kwa mchango wake kwenye jamii yetu. Binafsi naamini huu ni mwanzo tu wa mazuri mengi ambayo binti huyu halisi wa ki Tanzania anajaribu kufanya. Sekta ya kulea watoto ambao wamezaliwa kabla ya wakati inahitaji hela nyingi na kwasababu ambazo Mimi na wewe hatuzijui kumekua na vifaa VICHACHE sana vya kuwahifadhi watoto hao mara tu wanapo zaliwa. Doris na Foundation yake amekua akipigana vita hiyo kuhakikisha vifaa vinapatikana sio mjini tu, hata mikoani ili kuokoa maisha ya watoto hawa ambao wengine huishia kwenye debe la taka kwasababu tu walizaliwa kabla ya wakati wao. Yangu matumaini utamuelewa na utapata nafasi ya kumfuatilia na kama utakua na lolote ambalo unaweza kuchangia basi yuko kwenye mitandao ya kijamii maana siku hizi kumpata mtu na kujua ambacho anakifanya imekua rahisi kupitia mitandao hiyo. Mimi najivunia sana yeye na yangu matumaini atafanikiwa sana kwenye sekta hii kama nasi tutaweza kumsaidia pale panapowezekana. Tunahitaji kina Doris tele kwenye jamii yetu maana vya kusaidia viko vingi. Yangu matumaini episode hii itasaidia kukufungua macho kwenye mengi ambayo jamii yetu ina uhitaji. Love, Salama. --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support
More Episodes
Mfaume Mfaume ni yule mwana ambaye akitokea sehemu ni sahihi kwako kuwaambia wahusika kwamba jamani, mwamba huyu hapa! Muonekano wake pekee unamfanya mtu ajue yuko kwenye presence na mtu maalum na baadae ukishajua hasa nini anafanya basi huwezi ku doubt yote ambayo utaambiwa juu yake lakini kubwa...
Published 03/02/23
Published 03/02/23
Toufiq ni moja ya majina makubwa kati ya wafanya biashara wazuri na sasa mwanasiasa na Mbunge wa Mpendae, kwa wazee na vijana wa visiwani humo yeye ni mmoja wa mifano ya kuigwa ingawa kwake yeye yaliyo mengi kwenye maisha yake ni nguvu kubwa ilifanywa na Marehemu Mzee wake Ndugu Salih Hassan...
Published 02/23/23