SE7EP21 - SALAMA NA BILLNASS | MJUKUU
Listen now
Description
Katika pita pita zangu siku si nyingi nilimsikia mtu akimzungumzia mgeni watu wa wiki hii kwamba ni ‘Jay Z’ wa Bongo na si kwasababu kamuoa mmoja wa wasanii hodari wa kike na ambao wako juu ki muziki, ila pia akili yake ya kibiashara kwa kiasi kikubwa imemfanya yeye aone hivyo. Kwa ufahamu wangu niliambiwa na kushuhudia suala la maneno na mawazo ‘kuumba’. Pale mtu au watu wanapo kuona na ukichanganya na juhudi zako na nia na madhumuni ya wewe kutaka kufika pale basi mengine kutimia huwa ni suala la wakati tu. Hivyo pia ndivyo ambavyo mimi namuona Ndugu William Nicholaus Lyimo almaaruf Bill Nass. Mara yangu ya kwanza kukutana nae uso kwa macho ni miaka kama sita au saba iliyopita wakati nafanya kipindi cha Ngaz kwa Ngaz special edition. Ambacho mimi na Josh Murunga tulikua tunafanya ilikua kuwapa nafasi wasanii hodari kuwa ma host wa countdown hiyo ya ngoma zao kali 20 kwa wakati huo na kuzitolea maelezo yake. Kwa Bill Nass ilikua kama kumtafuta Kuku tu, yaani RAHISI sana. Alikua natural wataalam wanasema, kuanzia matamshi (haya wengi huwashusha hadhi kwa kiasi flani) mpaka swagg ambayo mtangazaji anatakiwa awe nayo kwake ilikua ipo. Kuvaa kwake, kuheshimu wakati na kuskiliza maelekezo na kisha kuyafanyia kazi ilikua 100, na mimi kwenye hili nilikua mtazamaji tu, kazi kubwa aliifanya Ndugu Josh akiwa kama Director. Yangu matumaini Bill Nass siku moja atataka kufanya kitu kama kile maana kitamfaa mno na itakua moja ya income zake nyingi ambazo anazo. Kwake yeye kuamua kumuoa mmoja ya wasanii hodari wa kike ambaye ana mashabiki wengi na pengine wengi wao ni wanaume nadhani lilikua si amuzi mdogo kwao wote wawili. Wawili hawa mahusiano yao yalikua hadharani kwa sote kuyaona na kuwa na maoni nayo. Kuanzia ku leak kwa video yao ya faragha mpaka mahusiano ya mkewe na Marehemu Ruge, kila kitu kilikua nje nje. Je haya yaliathiri au kuyajenga mahusiano yao kwa kiasi gani? Vipi kuhusu suala la Marehemu Godzilla ambaye kulikua na shutma kwamba alikua anauiga style yake na baadhi ya Radio zilikua zinampa nafasi yeye ili kumficha Zilla? Na je suala la kifo chake ambalo lilimleta yeye karibu na mtoto wa Zilla? Hii ilikua inamsumbua vipi wakati watu wanasema hivyo? Na je alikua anaona jinsi ambavyo ilikua inamsumbua Zilla? Ukiachana na muziki Nenga pia ni mfanyabiashara mzuri tu ambaye amekua akitumia jina lake ipasavyo ili kuweza kujitengenezea kipato cha pembeni ambacho ni cha uhakika zaidi kuliko mziki ambao anafanya. Nna uhakika na yeye anajua kwamba ana uhakika wa kuuza electronics zaidi kwa mara nyingi kuliko uhakika wa kuwa na hit song nyingi kwa mwaka. Na hiyo haimaanishi kama yeye si msanii HODARI ila zaidi kwenye suala la wimbo kuwa mzuri lakini watu wasiupokee kama matarajio yanavyokua. Humu pia tulichambua kiasi kuhusu jina lake ambalo amelirithi. Majukumu, biashara, mapenzi, urafiki, usia na familia. Ningependa u enjoy kama ambavyo sisi tu enjoy wakati tunaongea. Love, Salama. --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support
More Episodes
Mfaume Mfaume ni yule mwana ambaye akitokea sehemu ni sahihi kwako kuwaambia wahusika kwamba jamani, mwamba huyu hapa! Muonekano wake pekee unamfanya mtu ajue yuko kwenye presence na mtu maalum na baadae ukishajua hasa nini anafanya basi huwezi ku doubt yote ambayo utaambiwa juu yake lakini kubwa...
Published 03/02/23
Published 03/02/23
Toufiq ni moja ya majina makubwa kati ya wafanya biashara wazuri na sasa mwanasiasa na Mbunge wa Mpendae, kwa wazee na vijana wa visiwani humo yeye ni mmoja wa mifano ya kuigwa ingawa kwake yeye yaliyo mengi kwenye maisha yake ni nguvu kubwa ilifanywa na Marehemu Mzee wake Ndugu Salih Hassan...
Published 02/23/23