Nchi zote pamoja na mashirika ya kimataifa ikiwemo UN yanawajibika kukomesha ukaliwaji wa Palestina
Listen now
Description
Tume hiyo huru imeyasema hayo katika taarifa mpya ya msimamo wa kisheriia iliyotolewa mjini Geneva Uswis kuhusu eneo linalokaliwa la Palestina ikiwemo Jerusalem Mashariki ambayo imeweka wazi maoni ya tume kuhusiana na wajibu wa serikali na jinsi Baraza Kuu na Baraza la Usalama linavyoweza kutambua na kutekeleza mbinu na hatua sahihi zinazohitajika kwa kazi hiyo hadi mwisho wa ukaliwaji huo, na kwa haraka iwezekanavyo. Tume ihiyo imebaini kwamba maoni ya ushauri ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki kuhusu matokeo ya Kisheria yanayotokana na sera na desturi za Israel katika eneo linalokaliwa la Palestina ikiwa ni pamoja na Jerusalem Mashariki ni wenye mamlaka na usio na utata kwa kusema kwamba kuendelea kuwepo kwa Israel katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu ni kinyume cha sheria na sheria ya kimataifa. Taarifa hiyo ikitolewa Geneva Gaza kwenyenyewe hali inaendelea kuwa tete, kwa mujibu wa Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestinna UNRWA Phillipe Lazzarini, kwani shule nyingine ya UNRWA imeshambuliwa leo Jabalia Kaskazini mwa Gaza, watu kadhaa wameripotiwa kuuawa na miongoni mwao Watoto wengi waliokuwa wakipata hifadhi katika jengo hilo. Lazzarini amesema hili ni shambulio la tatu dhidi ya majengo ya UNRWA kwa wiki moja. Na pia wafanyakazi wa shirika hilo wanaendelea kuuawa sasa wameffikia 231 tangu kuanza kwa vita hii Oktoba mwaka jana. Naye msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF James Elder akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi hii leo amesema “Gaza ni mfano halisi wa ulimwengu wa kuzimu duniani kwa watoto milioni moja wa eneo hilo. Na hali inazidi kuwa mbaya, siku baada ya siku, tunapoona athari za kutisha za mashambulizi ya anga ya kila siku na operesheni za kijeshi za Israek kwa watoto wa Kipalestina.” Nalo shirika la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA likiangazia Ukingo wa Magharibi limesema “Vikosi vya Israel vimekuwa vikitumia mbinu mbaya za vita katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, na kuibua wasiwasi mkubwa juu ya matumizi ya nguvu kupita kiasi na kuongeza mahitaji ya kibinadamu ya watu.” Ameelezea wasiwasi kuhusu mashambulizi ya walowezi wa Israel dhidi ya Wapalestina na miti yao ya mizeituni wakati huu wa mavuno ya kila mwaka.
More Episodes
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Geneva Uswisi kuwasikia vijna kutoka Kenya ambao wanashiriki kongamano la vijana, wakieleza kuhusu mkataba wa zama zijazo na mchango wao katika kuutekeleza mashinani mwao. Pia tunakuletea muhtasari wa habar iza Sudan, Kura ya Knesset kuhusu...
Published 10/29/24
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, (WFP) leo kwa mara nyingine tena limetahadharisha kwamba bila msaada wa kibinadamu nchini Sudan, mamia ya maelfu wanaweza kufa kwa njaa.  Vita vya kikatili nchini Sudan vimesababisha janga kubwa zaidi la njaa duniani, imeandika WFP katika...
Published 10/28/24