Mlo shuleni ulibadilisha maisha yangu- Mkurugenzi wa WFP Somalia
Listen now
Description
Kila siku, mamilioni ya watoto kote ulimwenguni huenda shule wakiwa na njaa, wengi wao wakiteseka na utapiamlo sugu ambao huathiri ukuaji wa kiakili na utendaji wao katika masomo. Wanaobahatika huweza tu kumaliza masomo yao na kufanikiwa maishani kutokana na programu ya ‘mlo ya shuleni’ inayoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula Duniani (WFP). Mfano wa wanufaika hao ni El-Khidir Daloum, Mkurugenzi wa sasa wa WFP nchini Somalia.  "Mimi ni zao la mlo wa shule," hayo ni maneno ya El-Khidir Daloum ambaye ana shukrani tele kwa WFP kwa kuendesha programu ya ‘mlo shuleni’ iliyomfaidisha  alipokuwa mwanafunzi. Hivi sasa, akiwa Mkurugenzi wa WFP nchini Somalia, Daloum ameweka dhamira ya kazi yake kuhakikisha upatikanaji wa chakula kwa wote. Je Daloum aliifahamu vipi programu ya mlo shuleni ya WFP kwa mara ya kwanza? “Tulipofika pale, tukakuta ni shule ya bweni, wakati huo wazazi wetu hawangeweza kugharamia shule hiyo. Kwa hivyo, shule ilifanya ushirikiano kati ya serikali na Shirika la Umoja wa Mataifa Chakula Duniani (WFP). Na hiyo ndiyo ilikuwa mara yangu ya  kwanza kuonja dagaa wa Kijapani, maziwa ya unga kutoka Uholanzi, na jibini ya Denmark, yote yaliletwa kwetu kupitia mlo wa shule.” Je Daloum anadhani maisha yake yangekuwa vipi kama WFP isingetoa mlo shuleni? “Nikiwaza kuhusu kizazi changu, hasa wale waliokuwa katika shule za bweni, bila ushirikiano huo kati ya serikali ya nchi yangu na WFP, hatungeweza  kumaliza elimu yetu. Ndio maana nakwambia kwamba mimi ni zao la mlo shuleni kutoka kwenye shule ya msingi kwenda katika shule ya kati na hatimaye sekondari, yote haya matatu yalifaulu kutokana na mlo shuleni.”
More Episodes
Kaunti ya Turkana Kaskazini mwa Kenya moja ya maeneo kame mradi wa ufugaji nyuki wa WFP umekuwa mkombozi kwa wakulima walioathirika na mabadiliko ya tabianchi. Katika kaunti hii vumbi linalotimuka katika eneo tambarare lisilo na miti linakufanya kujiuliza je Nini kizuri kinaweza kufanyika hapa...
Published 10/21/24
Hii leo jaridani tunaangazia mkutano wa COP16 katika mji wa Santiago de Cali au Cali huko nchini Colombia na ufugaji nyuki Turakana nchini Kenya. Pia tunakupeleka nchini Somalia kufutilia programu wa WFP wa mlo shuleni na mashinani inatupeleka nchini Lebanon. Mkutano wa 16 wa nchi wanachama wa...
Published 10/21/24