21 OKTOBA 2024
Listen now
Description
Hii leo jaridani tunaangazia mkutano wa COP16 katika mji wa Santiago de Cali au Cali huko nchini Colombia na ufugaji nyuki Turakana nchini Kenya. Pia tunakupeleka nchini Somalia kufutilia programu wa WFP wa mlo shuleni na mashinani inatupeleka nchini Lebanon. Mkutano wa 16 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa bayonuai (COP16) umeng’oa nanga leo katika mji wa Santiago de Cali au Cali huko nchini Colombia ambapo mataifa 196 yatajadili jinsi ya kusitisha na kubadili mwelekeo wa kudorora kwa ulimwengu wa asili.Kila siku, mamilioni ya watoto kote ulimwenguni huenda shule wakiwa na njaa, wengi wao wakiteseka na utapiamlo sugu ambao huathiri ukuaji wa kiakili na utendaji wao katika masomo. Wanaobahatika huweza tu kumaliza masomo yao na kufanikiwa maishani kutokana na programu ya ‘mlo ya shuleni’ inayoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula Duniani (WFP). Mfano wa wanufaika hao ni El-Khidir Daloum, Mkurugenzi wa sasa wa WFP nchini Somalia.Makala inatupeleka Kaunti ya Turkana Kaskazini mwa Kenya moja ya maeneo kame ambako mradi wa ufugaji nyuki wa WFP umekuwa mkombozi kwa wakulima walioathirika na mabadiliko ya tabianchi.Mashinani fursa ni yake Waffiyah Diyah kutoka Lebanon ambaye ni muathirika wa vita vilivyolazimisha maelfu ya watu kufangasha viragoanaelezea hali ya familia yake baada ya kukimbia mashambulizi na kupoteza kila kitu, lakini sasa anapokea msaada kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM).Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
More Episodes
Umoja wa Mataifa unaendelea kuunga mkono serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC katika kukabili habari potofu na za uongo hususan huko mashariki mwa nchi ambako vikundi vilivyojihami vinaendelea kushambulia raia na kupambana na jeshi la serikali. Hivi karibuni Umoja wa Mataifa kupitia...
Published 10/22/24
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini DRC kufuatilia kazi za kituo cha Taifa cha Redio na Televisheni, RTNC huko Beni jimboni Kivu Kaskazini za kakabiliana na habari potofu. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani. Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo...
Published 10/22/24
Kaunti ya Turkana Kaskazini mwa Kenya moja ya maeneo kame mradi wa ufugaji nyuki wa WFP umekuwa mkombozi kwa wakulima walioathirika na mabadiliko ya tabianchi. Katika kaunti hii vumbi linalotimuka katika eneo tambarare lisilo na miti linakufanya kujiuliza je Nini kizuri kinaweza kufanyika hapa...
Published 10/21/24