Description
Hii leo jaridani tunaangazia mashambulizi ya Israeli kaskazini mwa Gaza unaoleta changamoto za kuendelea na chanjo ya polio, na virusi vya Marburg nchini Rwanda. Makala tunakupeleka nchini Uganda na mashinani nchini Lebanon, kulikoni?
Mashambulizi makali ya anga kutoka kwa jeshi la Israel, idadi kubwa ya watu kutawanywa na ukosefu wa fursa ya kufika Gaza Kaskakzini vimelazimisha kuahirishwa kwa kameni ya chanjo kwa mujibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Afya Duniani WHO, la kuhudumia watoto UNICEF na la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWAMkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani amewapongeza wahudumu wa afya wa nchini Rwanda kwa kazi kubwa wanaoyoifanya kukabiliana na ugonjwa wa Marburg. Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus ameeleza hisia zake hizo mwishoni mwa wiki alipofanya ziara katika vituo mbalimbali vya afya katika mji Mkuu wa nchi hiyo, Kigali.Ndoa za utotoni,ubakaji na kutelekeza watoto, haya ndio matatizo yaliyokuwa yanaripotiwa mara nyingi zaidi kwa kuathiri watoto katika makazi ya wakimbizi katika wilaya Kyegegwa magharibi mwa Uganda. Hata hivyo, kwa msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto UNICEF na ufadhili kutoka wahisani wa Uingereza UKaid, maelfu ya wazazi katika makazi ya wakimbizi na jamii zinazohifadhi waakimbizi katika wilaya ya Kyegegwa wamepewa mafunzo juu ya malezi bora ili kuondoa ukatili dhidi ya watoto, wanawake, na wasichana.Mashinani tunabisha hodi Lebanon, kumsikia Farah, Mkimbizi wa ndani anayepokea msaada kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, baada ya kujifungua kwenye hema, akieleza alichokabiliana nacho.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Geneva Uswisi kuwasikia vijna kutoka Kenya ambao wanashiriki kongamano la vijana, wakieleza kuhusu mkataba wa zama zijazo na mchango wao katika kuutekeleza mashinani mwao. Pia tunakuletea muhtasari wa habar iza Sudan, Kura ya Knesset kuhusu...
Published 10/29/24
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, (WFP) leo kwa mara nyingine tena limetahadharisha kwamba bila msaada wa kibinadamu nchini Sudan, mamia ya maelfu wanaweza kufa kwa njaa.
Vita vya kikatili nchini Sudan vimesababisha janga kubwa zaidi la njaa duniani, imeandika WFP katika...
Published 10/28/24